27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa kuongoza harambee ya vituo vya afya Mwanza

Na Sheila Katikula, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vituo vya afya vipya Saba inayotarajiwa kufanyika Julai 30, mwaka huu kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya harambee inayotarajiwa kufanyika Julai 30, mwaka huu katika uwanja wa Nyamagana.

Hayo yamebainishwa Alhamisi Julai 28, 2022 na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) mkoani humo.

Amesema lengo la harambee hiyo ni kusaidia Serikali katika kutoa huduma kwa jamii nakuongeza kuwa itaisaidia Serikali kutoa huduma kwa wananchi.

“Bakwata Mkoa wa Mwanza tumeandaa harambee kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vituo saba vipya vya afya ndania ya mkoa wetu wa Mwanza na katika shughuli hiyo tunatarajia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa takuwa mgeni rasmi.

“Hivyo, tunaomba kuwaarika dini zote kujitoa na kujitolea michango ya ujenzi wa vituo vya afya Saba ambavyo vipo katika wilaya ya Ilemela, Nyamagana, Magu, Ukerewe, Misungwi, Kwimba na Sengerema.

“Tunapokea mchanga, kokoto, nondo, saruji na kitu chochote ambacho kitatusaidia kwenye Ujenzi hata kama mtu anataka kutusaidia kwanzia msingi hata kumaliza jengo lote tupo tayari,” amesema Kabeke.

Naye Sheikh wa Wilaya ya Nyamagana, Othuman Ndaki amewaomba wazazi na walezi kuwapa watoto wao sadaka ili waweze kutoa kwenye harambee hiyo ambayo itatengeneza historia kwa kuvuka malengo.

Kwa upande wake Mshauri wa Sheikhe Mkuu wa Mkoa Mwanza, Alhaji Swaleh Banyanga ambaye pia ni mfanyabiashara amewaomba waumini wa dini zote wenye uwezo kujitoa katika kujenga vituo vya afya kusaidia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles