23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Makamba: Kwa mara ya kwanza Tanzania tunaleta umeme wa joto ardhi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Serikali imeamua kuweka nguvu katika uzalishaji wa umeme wa njia mbalimbali ili kujitosheleza katika nishati hiyo muhimu.

Makamba ameyasema hayo leo Julai 28, kupitia ziara yake ya siku 21 ya Kijiji kwa Kijiji amefika kwenye Kijiji cha Iramba Kata ya Ntaba Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya na kukagua ujenzi wa miundombinu ya Umeme wa Joto ardhi.

“Serikali imeamua sasa kuweka nguvu katika kuzalisha umeme kwa njia mbalimbali, tuna umeme wa Maji, Umeme wa Gesi na safari hii tumewekeza kwenye umeme wa Joto ardhi, Tuko hapa Rungwe tuna uwezekano wa kuzalisha umeme wa Joto ardhi.

“Katika Bajeti tunayoendelea nayo tumewekeza Sh bilioni 5 kwa ajili ya kuendelea miradi hii, tumenunua mtambo maalum wa kuchoronga mpaka Kilometa 3 chini ili kuweza kulifikia joto ambalo litatoa mvuke utakaozungusha mtambo wa kuzalisha umeme ni mradi muhimu kwetu, tunayo maeneo mengi Tanzania yenye fursa ya kuzalisha umeme wa namna hii kuliko kiwango cha umeme tulichonacho sasa hivi nchini.

“Ni muhimu kwenye Gridi ya Taifa kuwe na mchanganyiko stahiki, ili chanzo kimoja kikileta shida labda mvua zikigoma kuwe na umeme wa chanzo kingine, Joto ardhi haina hali ya hewa hii ni muda wote, Tunategemea 2025 tutakua tumezalisha Megawati 200 kwa kuanzia lakini mbele tunakoelekeza tutazalisha zaidi,” amesema Waziri Makamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles