26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AWATAKA WAWEKEZAJI KUFUATA SHERIA

Na Mwandishi Maalumu

-UFARANSA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka watu wote wenye nia ya kutaka kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania, kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais (Uendelezaji Bishara) wa Kampuni ya PIRIOU, Michel Perrin.

Waziri Mkuu amekutana na Perrin jijini Paris nchini Ufaransa, kupitia ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambapo Kampuni ya PIRIOU inataka kuja nchini kuwekeza katika utengenezaji na ukarabati wa meli.

Akizungumza na mwekezaji huyo, Waziri Mkuu alimshukuru kwa nia yake ya kutaka kuwekeza nchini, ambapo alimtaka afuate sheria, kanuni na taratibu za uwekezaji nchini.

“Tanzania ni sehemu nzuri ya uwekezaji kwa sababu kuna fursa nyingi. Pia ni nchi yenye amani na utulivu wa kisiasa pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji, hivyo nakukaribisha sana,” alisema.

Kwa upande wake ,Perrin alisema ameamua kuja kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi salama na kwamba ana uhakika wa kupata soko ndani ya nchi pamoja na mataifa jirani.

Alisema anaamini uwekezaji wake nchini Tanzania utakuwa na tija, hivyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali na pia atahakikisha anafuata sheria zote za nchi.

Perrin alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Balozi Samwel Shelukindo, kutokana na ushirikiano anaompa kuhusu masuala ya uwekezaji nchini.

Naye Balozi Shelukindo amesema atahakikisha anaendelea kutafuta wafanyabiashara mbalimbali na kuwashawishi waje kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles