25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa awataka Lindi, Mtwara kuchangamkia kilimo cha muhogo

NA Mwandishi Wetu – Lindi

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara watumie fursa ya kiwanda cha kuchakata muhogo katika Kijiji cha Mbalala kwa kuongeza kasi ya kulima zao hilo kwa wingi ili wajiongezee kipato.

“Kama unataka fedha nenda kalime muhogo kwa sababu kuna soko la uhakika na pia zao hili ni la muda mfupi na kilimo chake ni rahisi. 

“Kwa sasa hatuna muda wa kukaa vijiweni, vijana jiungeni katika makundi na muanzishe mashamba ya mihogo, soko lipo, tena mwenye kiwanda atawafuata huko huko shambani bila kujali umbali wa eneo zao hilo lipo,” alisema.

Majaliwa alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua kiwanda cha kuchakata unga wa muhogo cha Kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo Kijiji cha Mbalala mkoani hapa.

Pia alisema lengo la Serikali la kuhamasisha ujenzi wa viwanda ni kusaidia kuongeza thamani ya mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima kabla ya kuuzwa.

Alisema baada ya kuzinduliwa kwa kiwanda hicho, sasa wakulima wa zao hilo watakuwa na soko la uhakika.

 “Ni dhahiri kwamba wakulima wetu wa muhogo wanapaswa kulima kitaalamu kwa lengo la kuongeza uzalishaji, hivyo Wizara ya Kilimo ihakikishe wakulima wetu wanapata utaalamu wa kilimo cha kisasa cha muhogo,” alisema Majaliwa.

Hata hivyo, alisema licha ya kiwanda hicho, Serikali imefanikiwa kupata soko la zao hilo nchini China na hadi kufikia Januari, mwaka huu jumla ya kampuni tano zinazojihusisha na biashara ya muhogo zimetambulishwa nchini. 

Alisema hadi kufikia Februari, mwaka huu, Kampuni ya Dar Cantoni Investment imesafirisha tani 187 za muhogo mkavu (makopa) kwenda China na wanatarajia kusafirisha tani 2,060 ifikapo Juni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles