24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AWAONYA MA-DC, MA-DED

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa

 

 

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa wilaya wakurugenzi wa halmashauri nchini kuzingatia mipaka ya madaraka yao na kuhakikisha hatua wanazochukua katika utendaji wao zinafuata  sheria, kanuni na taratibu katika utumishi wa umma.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya.

Alisema  viongozi hao wanatakiwa kusimamia kwa ukamilifu nidhamu katika utumishi wa umma kwa sababu wenyewe ni kioo katika kuishi kwa kuzingatia miiko  ya utumishi.

Alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo na kuendelea kuwaimarisha zaidi katika kusimamia shughuli za Serikali na maendeleo kwenye maeneo yao.

  Waziri Mkuu pia amewataka viongozi hao kutoa kipaumbelea katika kufuatilia na kusimamia kwa makini sekta za afya, kilimo, elimu na maji kwa kuwa ndizo zinazogusa zaidi maisha ya wananchi .

“Simamieni na kuziba mianya yote ya upotevu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya na kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji na kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira katika maeneo yenu,” alisema.

Naye  Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Suleiman Jafo alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha viongozi hao wanapata mafanikio makubwa katika utendaji wao wa kazi   Serikali iweze kupata tija.

Awali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja,  alisema   mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi hao   kuwajengea uwezo wa kuongoza kwa kuwa mazingira ya kufanyia kazi na mbinu za kungoza zinabadilika.

Alisema mafunzo hayo yatatolewa kwa awamu nne kupitia kanda nne tofauti ambako awamu ya kwanza imeanza na kanda ya kati na imehusisha mikoa sita ya Dodoma, Kigoma, Katavi, Tabora, Morogoro na Singida

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles