26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Majabvi aiangukia Simba

Justice-MajabviNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MCHEZAJI wa kimataifa wa Simba, Justice Majabvi, ameuomba uongozi wa klabu hiyo kumpa nafasi nyingine ya  kuendelea kuichezea timu hiyo katika mechi zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Majabvi ambaye ni raia wa Zimbabwe alitishia kuondoka katika timu hiyo kwa madai kuwa uongozi umeshindwa kumtimizia mahitaji yake ya msingi.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo zililipasha MTANZANIA jana kuwa, Majabvi aliwapigia simu viongozi wa timu hiyo kuomba ajiunge na timu mkoani Shinyanga.

Chanzo hicho kilisema, uongozi umepanga kufanya mazungumzo na mchezaji huyo kwanza kabla ya kumruhusu kuendelea kuichezea timu hiyo.

“Unajua huyu mchezaji ametudhalilisha sana, ameukosea heshima uongozi wa Simba, kipindi chote alikuwa anajiona yupo sahihi kwa yale anayoyaongea katika vyombo vya habari.

“Sasa amegundua kosa lake anapiga simu kuomba asafiri aje kujiunga na timu, hilo halitawezekana hadi tutakapozungumza naye,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilieleza kuwa hatua aliyofikia Majabvi anapaswa kuomba  radhi kwani vitu vingi alivyozungumza ni uongo.

Majabvi alishindwa kujiunga na kikosi cha Simba kilichoelekea Mwanza kucheza dhidi ya Toto Africans, kwa madai kwamba haridhishwi na namna timu hiyo inavyoendeshwa.

Kikosi cha Simba jana kilitarajia kuvaana na timu ya Geita katika mchezo wa kirafiki, ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC Jumamosi hii, Uwanja wa Kambarage.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles