26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKIMU WAGAWIWA KOMPYUTA MPAKATO

JOHANES RESPICHIUS Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

SERIKALI imeanza kutekeleza mpango wa kugawa kompyuta mpakato kwa mahakimu wote nchini zitakazowawezesha kuandaa wenyewe hati za hukumu  kuepuka ucheleweshwaji wa hati hizo baada ya kesi kumalizika.

Jaji Kiongozi, Frednand Wambari, alikuwa akizungumza   Dar es Salaam jana wakati wa kuhitimisha maonyesho ya Wiki ya Sheria.

Alisema mpango huo umeanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam ambako Serikali imetoa kompyuta 58.

Jaji Wambari alisema mpango huo utakuwa wa nchi nzima ukiwa na lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za mahakama na kupunguza mrundikano wa mashauri mahakamani.

“Umekuwapo ucheleweshwaji wa hati za hukumu katika ngazi zote kuanzia mahakama za mwanzo, wilaya, Hakimu Mkazi, Mahakama kuu na za Rufani.

“Ili kuondoa tatizo hili tutaanza kutoa kompyuta mpakato kwa mahakimu 58 wa Mkoa wa Dar es Salaam.

“Baada ya hapo mpango huu utasambaa nchi nzima   lengo likiwa ni kuharakisha utoaji wa hukumu kwa kesi zilizo tayari,” alisema Jaji Wambari.

Naye  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, alisema mahakama imejipanga kuongeza kasi ya utoaji wa haki kwa wakati, vitendea kazi, rasilimali watu na kutoa hati za hukumu kwa haraka.

Alisema ili kuhakikisha huduma za mahakama zinawafikia wananchi wengi hususan wanaoishi vijijini ambao wengi wao ni wakulima na wafugaji, Serikali imepanga kuanzisha mahakama zinazotembea ambazo zitaharakisha utoaji wa huduma.

“Serikali imepanga kuanzisha mahakama ndogo zaidi ambazo zitatoa huduma kwa urahisi kwa kuwafikia wananchi wengi.

“Hiyo ni kwa sababu kumekuwa na changamoto kubwa ya upungufu wa mahakama za mwanzo ambako mpaka sasa zipo mahakama za mwanzo zisizozidi 75 ikilinganishwa na kata zaidi ya 3000 nchini.

“Kwa hiyo  kutakuwa na mahakama zinazotembea katika mabasi na boti,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles