26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yatoa hati ya kumkamata Wema Sepetu kwa kuruka dhamana

KULWA MZEE DAR ES SALAAM

Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu yuko matatani baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa hati ya kumkamata  kwa kuruka dhamana.

Wema anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza  video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.

Hati hiyo ya kumkamata Wema imetolewa leo Juni 11 mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonda, baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Silvia Mitanto kudai kwamba mshtakiwa hayuko mahakamani na hakuna taarifa yoyote.

Wakili wa utetezi, Ruben Simwanza, amedai mshtakiwa alifika Mahakamani lakini kaumwa hivyo ameshindwa kuingia katika chumba cha Mahakama.

Akitoa uamuzi Hakimu Maira amesema Mahakama inatoa hati ya kumkamata mshtakiwa kwa sababu kama alifika alishindwa nini kuingia mahakamani.

Wema anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono katika mtandao wa kijamii.

Wema anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhui.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles