LOUISVILLE, England
MASHABIKI wa gwiji wa masumbwi duniani, marehemu Muhammad Ali, wamekamilisha safari ya bondia huyo kwa kutoa salamu zao za mwisho kabla ya kushuhudia akipumzishwa katika makazi yake ya milele.
Takribani mashabiki 18,000, viongozi kutoka sehemu mbalimbali duniani na watu maarufu walikusanyika nyumbani kwa bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu, Louisville, Kentucky kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo.
Mara baada ya kukamilisha zoezi la kuuaga mwili wa bondia huyo, zoezi la kuuzika lilifanyika katika makaburi ya Cave Hill yaliyopo Ireland ya Kaskazini.
Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, alishiriki katika maziko hayo ambapo alisoma ujumbe maalumu kumhusu Ali. Mjane wa bondia huyo, Lonnie pamoja na watoto wake wawili kati ya tisa, Rasheda na Maryum, nao walikuwepo kwa ajili ya kumuaga kipenzi chao.
Mabingwa wa zamani wa masumbwi, Mike Tyson na Lennox Lewis, walibeba jeneza lenye mwili wa gwiji huyo, ambapo walishirikiana na mwigizaji Will Smith, ambaye alicheza filamu ya maisha ya Ali mwaka 2001.
Wakongwe wengine zaidi katika masumbwi, George Foreman na Larry Holmes, nao walibeba jeneza la Ali.
Wengine waliotarajiwa kuhudhuria mazishi hayo ni mwigizaji wa Marekani, Billy Crystal na mtoto wa kike wa Malcolm X, Attallah Shabazz pamoja na mfalme wa Jordan, Abdullah II.