26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Maradona: Messi ni mtu mzuri, hana utu

Lionel Messi
Lionel Messi

PARIS, UFARANSA

MKONGWE wa soka duniani na timu ya taifa ya Argentina, Diego Maradona, amedai kuwa Lionel Messi amekosa tabia ya kuwa kiongozi katika chumba cha kubadilishia nguo cha timu ya Taifa  ya Argentina kwenye michuano ya Copa America.

Maradona alimshambulia mshambuliaji huyo nyota wa klabu ya soka ya Barcelona, wakati akijadili juu ya ubora wa mchezaji huyo kwenye michuano ya Copa America akiwa na nguli mwenzake  wa taifa la Brazil, Edson Nascimento ‘Pele’.

Maradona anaangaliwa kama mfano wa kuigwa wa taifa hilo zaidi kutokana na mafanikio yake kwenye soka hasa wakati alipofikisha michezo 91 ya kimataifa akiwa na timu ya taifa mwaka 1977 na 1994.

Kutokana na ubora wake, nguli huyo anaona kwamba haoni usimamizi na umiliki wa Messi katika soka la taifa hilo.

Wakiwa kwenye mahojiano hayo, Pele (75), alimuuliza mshindi mwenzake wa Kombe la Dunia, Maradona (55), kama anamjua mchezaji huyo kwenye kikosi cha taifa ya Argentina mwenye uzalendo.

Hata Maradona alisema kwamba, hakuna ubishi kwamba Messi ni mchezaji mzuri lakini hana utu kutokana na kusumbuliwa na mafanikio binafsi zaidi ya taifa lake.

Maradona alisema kuwa Messi alifanikiwa kufunga mabao 50 katika michezo 107, lakini alipoteza fainali mbili za Copa America ambapo msimu uliopita taifa la Chile liliibuka na ubingwa huo.

Pia Maradona akaongeza kuwa miongoni mwa makombe makubwa yalipita machoni mwa Messi ni pamoja na Kombe la Dunia la mwaka 2014 nchini Brazil na Olimpiki ya mwaka 2008 ambalo aliambulia kupata medali ya dhahabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles