24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

MADIWANI WAHOFIA KUKUMBWA NA NJAA

Na Odace Rwimo

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora wanahofia kukumbwa na balaa la njaa endapo wataruhusu mazao ya chakula kuuzwa nje ya wilaya hiyo.

Hofu hiyo imeibuka katika baraza la madiwani hivi karibuni baada ya kupata taarifa za walanguzi wa mazao ya chakula kutoka mikoa jirani na kusababisha wizi katika mashamba ya mahindi.

Diwani wa Kata ya Kalola, Abdalllah Koni

(CCM), alisema wapo baadhi ya wafanyabiashara kutoka mikoa mingine waliofika  kununua mahindi kwa bei kubwa na kusababisha wizi.

Alisema kama serikali ya wilaya haitachukua tahadhari mapema ya kuzui kuuzwa   nafaka hizo wilayani hapo kutazuka balaa la njaa ambalo litasababisha madiwani kuhangaika kutafuta namna ya kuwanusuru wananchi wao.

Alisema  mavuno katika wilaya hiyo kwa mwaka huu  yamekuwa chini ya kiwango kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na   mvua isiokidhi mahitaji ya kilimo.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Shabani Katalambula, alisema kuna kila sababu ya kutoa tamko kama serikali, ya kuzui uuzaji wa chakula nje ya wilaya hiyo.

Alisema familia nyingi hazikupata chakula cha kutosha  hivyo kama serikali haitaingilia kati na kutoa mashariti makali kwa wafanyabiashara watapata wakati mgumu  kuwasaifia wananchi wa wilaya hiyo.

  Mwenyekiti wa Halmashauri, Saidi Ntahodi alitoa kauli ya kusimamisha uuzwaji wa chakula nje ya Wilaya ya Uyui.

Aliagiza jeshi la polisi kuwakamata watu waote watakaojihusisha na uuzwaji wa chakula nje ya

wilaya hiyo.

Ntahodi alisema endapo mtu yeyote atabaininika kusafirisha chakula kutoka wilayani hapo bila idhini ya mkuu wa wilaya, hatua kali za sheria zitachukuliwa bila kujali cheo wala wadhifa wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles