22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

WAKANDARASI WALILIA SHERIA YA MANUNUZI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAKANDARASI  wamesema kutokufuatwa Sheria ya Manunuzi ya Umma, kumekuwa kikwazo kwa wengi wao kupata zabuni za ujenzi.

Kutokana na hali hiyo, wameomba taasisi husika zizingatia sheria hiyo kwa kila zabuni inayotolewa.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Consolata Ngimbwa, wakati akisoma maazimio ya mkutano wa mwaka wa mashauriano kwa wakandarasi uliofanyika mjini Dodoma.

Mkutano huo, uliofunguliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, uliandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), na ni wa kila mwaka ambapo wakandarasi hukutana na kuzungumzia changamoto zinazowahusu na kuziwasilisha serikalini.

Alisema wakandarasi wameazimia kuwa taasisi zinazotangaza zabuni lazima zizingatie sheria hiyo ili kuweka uwanja uliosawa kwa wakandarasi kuwania zabuni hizo kila zinazotangazwa.

Alisema pia kwenye mkutano huo  wameazimia kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), iendelee kutoa elimu yaa kodi ya zuio (withholding tax) kwa wakandarasi kwani wengi wao bado hawajaielewa vizuri.

Alisema CRB itaendelea kuratibu mafunzo ya wakandarasi kwa kanda na wameazimiaa kuwa wakandarasi wanapaswa kuzingatia maadili kazini na watekeleze miradi kwa ubora unaotakiwa kwenye mikataba yao.

Alisema wameazimia kuwa mamlaka zinazotoa zabuni zisitangaze zabuni kabla ya kupata fedha kwani ucheleweshaji wa malipo kimekuwa kikwazo kikubwa kwa ustawi wa wakandarasi nchini.

Alisema mapendekezo hayo yatawasilishwa serikalini siku chache zijazo na kwamba wakandarasi wanaamini kuwa serikali sikizo ya awamu ya tano itafanyia kazi mapema ili kustawisha shughuli za wakandarasi nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Joseph Nyamhanga, aliwataka wakandarasi nchini kuwafichua maofisa wa serikali ambao wamekuwa wakiwaomba rushwa ili wawapatie zabuni za ujenzi wa miradi.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kushirikiana kupambana na rushwa kwenye utoaji wa zabuni kwani imekuwa ikisababisha miradi kuchelewa ama kutekelezwa kwa kiwango cha chini.

Kuhusu madeni ya wakandarasi, Nyamhanga aliwathibitishia wakandarasi kuwa serikali ina nia njema ya kulipa madeni yote ya wakandarasi na kwa wakati.

Alisema kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 serikali ilitenga Sh trilioni 1.006 kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi wa ndani na kwamba miongoni mwa fedha hizo Sh bilioni 406 ni fedha zilizotoka kwenye mfuko wa barabara.

Naye Msajili wa Bodi ya CRB, Rhoben Nkori, aliwataka wakandarasi kuzingatia mafunzo waliyoyapata kwenye mkutano huo ili kuhakikisha kazi zao zinakuwa bora zaidi.

Alisema kufanyakazi kwa kuzingatia mikataba na waajiri wao kutawasaidia  kujenga uaminifu kwa serikali na kwa wateja wengine hivyo kuwasaidia kutekeleza miradi mingi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles