24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Madereva wa masafa marefu wahimizwa kutumia vituo vya maarifa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Madereva wa masafa marefu nchini wamehimizwa kuvitumia vituo vya Maarifa ya Kudhibi UKIMWI ili kupata huduma mbalimbali zinazolenga kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI(VVU).

Mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Pwani, Grace Tete akitoa taarifa ya hali ya VVU mKoani humo wakati wa ziara ya kikazi ya makamishina wa TACAIDS kwa lengo la kukagua miradi ya UKIMWI inayosimamiwa na TACAIDS.

Hayo yamebainishwa Juzi na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS, Dk. Hadwiga Swai baada ya kutembelea kituo cha Maarifa kilichoko Manyoni mkoani Singida.

Amesema lengo la kufunguliwa kwa kituo hicho Mwaka 2016 ni kuwasadia madereva wanaoendesha magari makubwa kupima VVU, kupata dawa za kufubaza makali ya vizuri vya Ukimwi(ARVs) iwapo wameishiwa walioambao tayari wamiehaanza kutumia ARV na huduma nyingine ikiwamo kutoa elimu ya kujikinga maambukizi ya VVU, kwa wakaazi waliojirani na kituo hicho.

“Kitengo hiki kimefanya vizuri Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) ameweza kukisajili kuwa Zahanati sasahivi wanapata dawa kutoka serikalini na mimi napenda kuishukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia vifaa tiba mbalimbali ikiwamo dawa, darubini vifaa vya maabara na wahudumu wa afya.

“Wito wangu kwa madereva kituo hiki kipo hapa barabarani wanaweza kupita hapa wakasimamisha gari kama wameishiwa dawa zikiwamo zile za kuwakinga na maambukizi ya HIV na wakazipata hapa. Vituo hivi vipo sehemu nyingi hivyo ni wajibu wao kuvitumia vizuri ili kuendelea kuwa salama na kupunguza maambukizi ya HIV,” amesema Dk. Swai.

Moja ya Kituo cha maarifa kinachotoa huduma ya VVU katika Halmashauri ya Chalinze kupitu uratibu wa TACAIDS.

Akitolea mfano wa kituo hicho cha Manyoni amesema kimekuwa cha kuigwa kutokana na usimamizi mzuri unaofanywa na Mkurugenzi kupitia Mganga Mkuu wa Wilaya(DMO) wananchi pamoja na TACAIDS.

“Kituo hiki pia kinatoa huduma za vipimo vya haraka, pia DMO kwa kushirikiana na wananchi wameweza kuunda bodi ya kukiangalia hatua ambayo imesaidia kukifanya kubaki salama, nimpongeze Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS (Dk. Leonard Maboko) kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuanzisha vituo hivi kwani vimesaidia kupunguza maambukizi na kusogeza huduma kwa walengwa,” amesema Dk. Swai.

Akizungumzia Vituo hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko amesema wameanzisha aina hiyo ya vituo katika maeneo mbalimbali ya barabara kuu nchini na kwamba vingi vimekuwa vikifanya vizuri huku akitoa wito kwa madereva.

“Tunafurahi kuona vituo hivi vikifanya vizuri kama ambavyo tulikusudia katika barabara ya Dar es Salaam-Tunduma, Morogoro Mwanza, hivyo niwahimize pia madereva kuvitumia vituo hivi,” amesema Dk. Maboko.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dk. Jerome Kamwela(aliyevaa suti nyeusi) akifafanua umuhimu wa miradi ya ujenzi wa vituo vya maarifa katika barabara ya Dar es salaam –chalinze-Tunduma –Zambia na barabra ya Dar es salaam –Chalinze  –Arusha-Kenya kwa Makamishina na watalaam waliotembelea miradi hiyo

Amesema kwa sasa vituo hivi vya maarifa vya kudhibiti UKIMWI vimejengwa katika Mikoa ya Dar es Salaam-Kurasini, Pwani-Chalinze, Morogoro -Dumila, Dodoma- Kongwa, Iringa- Ilula, Mbeya- Kyela na Songwe- Tunduma.

Vingine ni vya Singida-Manyoni, Shinyanga-Kahama na Handeni mkoani Tanga. Vituo vyote vipo katika maeneo ya kando kando ya barabara ambapokuna maegesho ya magari Makubwaili kurahisisha ufikiwaji wa Madereva katika vituo husika.

Hii ni ziara ya kikazi ya kamisheni ya ya TACAIDS yenye lengo la kukagua shughuli zinazotekelezwa na tume hiyo iliyoanzia katika Mkoa wa Pwani, Dodoma na Singida.
Aidha, Kamisheni ilitembelea mradi wa Timiza malengo ambao unalenga kuwafikia wasichana Balehe na wanawake vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24.

Akizungumza na baadhi ya wanufaika wa mradi huo waliokutana na Kamisheni aliwapongeza na kuwasihi kuendelea kuzalisha bidhaa na biashara walizozianzisha kwa ufanisi ili wasijekurudi nyuma lakini pia wajiunge katika vikundi ili waweze kupata mikopo ya Halmashauri kwakuwa tayari wana elimu ya ujasiriamali waliyoipata kwenye mafunzo ya Timiza Malengo.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bicha walionufaika na Mradi wa timiza malengo kupitia elimu ya kujikinga na maambukizi ya VVU na Stadi za maisha .

Kamisheni pia ilitembelea halmashauri ya Kondoa ambapo ilifika katika shule mbili ambazo walimu walipatiwa mafunzo hayo na vishikwambi yyenye vitini kwa lengo la kutoa elimu kwa vijana namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU na kubaki shule kuhakikisha wanamaliza shule salama.

Baadhi ya shule ambazo walimu walishiriki katika mafunzo ya Timiza malengo katika halmashauri ya Kondoa ni pamoja shule ya Msingi Iboni ambayo inawanafunzichanganyiko na wenye ulemavu pamoja na shule ya Sekondari Bicha.

Baada ya kutembelea shule hizo wanafunzi walionesha kuwa na uelewa wa kutosha namna ya kijikinga na maambukizi ya VVU na kuepuka vitedo vya kikatili wanavyoweza kutendewa katika Umri mdogo.

Mwenyekiti wa Kamisheni pia aliwasisitizia walimu kuendelea kutoa elimu hiyo kwa vijana kwakuwa elimu hiyo ikianzia mashuleni itakoa vijana waliowengi hata wanapomaliza shule wanakuwa tayari wanatambua namna kuendelea kuishi wakiwa salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles