27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Netta, Mr Eazi Waangusha Kolabo Kali ‘Playground Politica’

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MSANII maarufu wa muziki wa Pop, Netta amemshirikisha staa mkubwa wa muziki wa Nigeria, Mr Eazi katika ngoma mpya ya Playground Politica ambayo imeshaanza kuwa gumzo kutokana na ubunifu uliotumika, kuanzia kwenye mashairi mpaka kwenye video ya wimbo huo.

Netta ambaye amejipatia umaarufu mkubwa barani Ulaya, ameamua kuja kitofauti katika ngoma hiyo kwa kuchanganya ladha za Pop na Afrobeat ambapo tangu ngoma hiyo ilipoachiwa, mashabiki wamekuwa na maoni mengi kuhusu ubora wake

Netta ameeleza kwamba ameamua kumshirikisha Mr Eazi katika ngoma hiyo, ikiwa ni hatua yake ya kuenzi maisha yake ya utotoni, aliyoyaishi nchini Nigeria ambapo hata video ya wimbo huo, imefanyikia nchini Nigeria katika mazingira aliyoishi akiwa mtoto.

Mwanadada huyo ambaye alipotoka Nigeria alihamia nchini Israel, anaeleza kwamba ameamua kurudi nchini Nigeria kufanya ngoma hiyo kwa sababu ana historia kubwa na nchi hiyo tangu akiwa mdogo, akikumbuka jinsi alivyokuwa akifurahia maisha ya utotoni akiwa ‘kibonge’ mtukutu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles