24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Shirika la MDH lakabidhi pikipiki 76 kukabili Uviko-19 Bukoba

Na Renatha Kipaka, Bukoba

SHIRIRIKA lisilo la kiserikali MDH mkoani Kagera wamekabidhi pikipiki 76 kwa viongozi wa Mkoa wa Kagera zitakazogawiwa kwa maafisa afya ngazi ya jamii ili kurahisha zoezi la utoaji chanjo ya Uviko-19.

Mkuu wa Kagera Albart Chalamila(katikati) akikata utepe pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa MDH baada kukabiziwa pikipiki na Mkurugenzi wa Shirika hilo alievaa miwani.

Makabidhiano hayo yamefaywa leo Septemba 21, 2022 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila na kulishukuru shirika hilo kwa kutoa usafiri huo utakawasaidia Maafisa Afya kufanya kazi hiyo kwa urahisi huku akiwaomba wananchi kuendelea kijitokeza kuchoma chanjo ya Uviko-19 kwani bado ugonjwa huo upo na unaua.

Chalamila amewashukuru MDH kwa kazi wanazozifanya katika kuisaidia jamii: “Leo mmekabidhi pikipiki zitakazotumiwa na maafisa afya ili kuwafikishia huduma ya chanjo wananchi katika Manispaa yetu ya Bukoba mkoani Kagera.

“Nitumie nafasi hii , kuwasihi wananchi wa mkoa wa kagera muendelee kujitokeza kupata chanjo ya Uviko-19 katika vituo mbali mbali kwani mpaka sasa ambao wamechanja wanafikia asilimia 63 tu,” amesema Chalamila.

Aidha, amewataka viongozi wa mkoa wa Kagera hasa wenyeviti wa mitaa kuhakikisha wanatunza amani nakuepuka kuwa chanzo cha migogoro katika mitaa yao ili kusaidia wawekezaji kufanya kazi zao kwa amani bila ubaguzi wowote.

Upande wake Meya wa Manispaa ya Bukoba, Godson Rwegasila amewashukuru viongozi wote wa Serikali na Mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19 huku akiwasisitiza viongozi hao kutumia usafiri waliokabidhiwa kuzunguka kila eneo kutoa elimu pamoja na huduma ya chanjo kwa wananchi juu ya umuhimu wa chanjo hiyo.

“Manispaa yetu ya Bukoba bado tunaendelea kupokea wawekezaji, tunamshukuru Mungu kwa hilo, tunazo halmashauri nane katika mkoa wetu wa Kagera lakini manispaa ya Bukoba ndicho kioo cha mkoa wetu, hivyo niwaombe wawekezaji wazidi kuja hapa kuwekeza kwani bado vipo viwanja vya aina mbalimbali vinavyoweza kutumika katika uwekezaji,” amesema Rwegasila.

Kwa upande wake Afisa Takwimu katika kituo cha Azamzam, Jackson Venust kilichopo Manispaa ya Bukoba amesema kuwa watumishi wa afya walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya usafiri lakini kutokana na msaada uliotolewa na MDH utawasaidia kuwafikia wananchi wengi katika maeneo mbalimbali.

“Tulikuwa tunzanguka mwendo mrefu zaidi ya kilometa 12 kutoka kituo cha afya kilipo kuwafikia wananchi waliopo mitaa mingine, lakini pia tulikuwa tunapata changamoto ya kubeba vifaa kama masanduku ya chanjo pamoja na sindando hivyo kutokana na usafiri huu tuliopatiwa changamoto hizi tutakuwa tumeondokana nazo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles