RAYMOND MINJA IRINGA
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim ametoa onyo kali kwa madereva wa mabasi kuacha tabia ya kukimbiza magari kwa spindi kubwa hali inayohatarisha usalama wa abiria na kwamba wakishindwa kufanya hivyo leseni zao zitafungiwa au kufutwa.
Onyo hilo limekuja ikiwa ni siku chache tangu kuonekana kwa kipande
cha video ya magari mawili ya kampuni ya Happy Nation na Rugwe
yakionekana kushindana kukimbia bila ya kujali usalama
wa abiria waliowabeba.
Akizungumza na madereva wa mabasi yaendayo mikoani kwenye stendi ya
mabasi Igumbiro mkoani Iringa, Muslim alisema kuwa hatofumbia
macho wala kuvulimia Watanzania wakipoteza Maisha kutokana na uzembe wa dereva.
Muslim alisema kuwa hadi sasa madereva 13 wameshafungiwa na wengine kufutiwa leseni zao kutokana na makosa mbalimbali ya barabara na kuwataka madereva kutii sharia bila shuruti ili kulinda ugali wao.
Alisema kuwa hivi sasa kumekuwa na tabia ya madereva kubeti na mabosi
wao kuwa ni nani atawahi kufikasha basi kwa haraka kwenye mkoa
anaokwenda jambo ambalo linamchochea kuendesha gari kwa spidi kubwa ili awahi kufika na kuchukua fedha yake.
Aidha amewataka watu wa vikosi vya usalama barabarani kote nchini kuhakikisha wanawakamata na kuwafungia au kuwafutia lesini madereva wote watakaokiuka sheria za usalama barabarani ili kunusuru maisha ya Watanzania wasiokuwa na hatia.