30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Ruwasa Simiyu watoa vifaa vya kujikinga na corona

Derick Milton, Simiyu

Wakala wa usambazaji maji vijijini (Ruwasa) Mkoa wa Simiyu umetoa msaada wa vifaa vya kunawia mikono vitakavyotumika kwenye baadhi ya shule za sekondari na hospitali mkoani humo ili kujikinga na virusi vya corona.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Katibu Tawala wa mkoa huo, Jumanne Sagini Mhandisi wa Maji,  Mahobe Singu kwa niaba ya meneja wa mkoa amesema kuwa msaada huo umegharimu kiasi cha Sh. milioni 1.7.

Amesema kuwa Ruwasa wametoa vifaa hivyo kwenye sehemu ambazo zina mkusanyiko mkubwa wa watu ikiwemo shule na hospitali ikiwa na lengo la kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya virushi vya corona.

Amevitaja vifaa hivyo ni pamoja na kontena tano zikiwa na stendi zake za kunawa mikono kwa kutumia miguu kufungulia maji na sabuni zinazotumika bila ya kushika.

“Vifaa hivi tumeona kuvitoa kama mchango wetu kwa jamii katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu, vitapelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa, hospitali ya Wilaya ya Maswa na Shule ya Sekondari Dutwa,” amesema Mhandisi Singu.

Akipokea Vifaa hivyo Katibu tawala amehukuru wakala huyo kwa kuunga mkono juhudi za mkoa na serikali katika kupamba na ugonjwa wa corona ambao unatajwa kuwepo nchini.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,873FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles