30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Madereva wa mabasi wapewa onyo kukimbiza magari

RAYMOND MINJA IRINGA

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim ametoa onyo kali kwa madereva wa mabasi  kuacha tabia ya kukimbiza magari  kwa spindi kubwa hali  inayohatarisha usalama wa abiria na kwamba wakishindwa kufanya hivyo leseni zao zitafungiwa au kufutwa.

Onyo hilo limekuja ikiwa ni siku chache tangu kuonekana kwa kipande

cha video ya magari mawili ya kampuni ya Happy Nation na Rugwe

yakionekana kushindana kukimbia bila ya kujali usalama

wa abiria waliowabeba.

Akizungumza na madereva wa mabasi yaendayo mikoani kwenye stendi ya

mabasi Igumbiro mkoani Iringa, Muslim alisema kuwa hatofumbia

macho wala kuvulimia Watanzania wakipoteza Maisha kutokana na uzembe wa dereva.

Muslim alisema kuwa hadi sasa madereva 13 wameshafungiwa na wengine  kufutiwa leseni zao kutokana na makosa mbalimbali  ya barabara na kuwataka madereva kutii sharia bila shuruti ili kulinda ugali wao.

Alisema kuwa hivi sasa kumekuwa na tabia ya madereva kubeti na mabosi

wao kuwa ni nani atawahi kufikasha basi kwa haraka  kwenye mkoa

anaokwenda jambo ambalo linamchochea kuendesha gari kwa spidi kubwa ili awahi kufika na kuchukua fedha yake.

Aidha amewataka watu wa vikosi vya usalama barabarani kote nchini kuhakikisha wanawakamata na kuwafungia au kuwafutia  lesini madereva wote watakaokiuka sheria za usalama barabarani ili kunusuru maisha ya Watanzania wasiokuwa na hatia.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles