32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Madereva wa gari, pikipiki watakiwa kuzingatia alama za barabarani, kufichua uhalifu


Na Malima Lubasha, Serengeti

MADEREVA wa Magari na Pikipiki katika Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara,wametakiwa kuheshimu ala ma za barabarani na kufichua waharifu wanaotumia vyombo hivyo kufanyia uharifu na wale wanaohari bu miundo mbinu ya barabara.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa kituo cha Polisi Mugumu, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, ASP Edward Ndayambugwa kwa niaba ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Serengeti, SSP Mashaka Mwikwabe wakati akifunga ma funzo ya siku10 ya udereva wa magari na pikipiki kwa washiriki zaidi ya 200 na kutunukiwa vyeti yaliyofa nyika  Serengti.

Amesema mafunzo hayo waliyopata yatawajengea uwezo wa kutumia vyombo vya moto kwa uadilifu na kuzingatia alama za barabarani ikiwa ni pamoja na kufichua waharifu wanaotumia vyombo hivyo kwa ma tukio mbalimbali ya kiharifu.

“Muda umefika sasa madereva wa gari na pikipiki mliopata mafunzo kushirikiana na Serikali kuwafichua wanaojihusisha na vitendo vya kiharifu na kuendesha mwendo kasi ili tuweze kuvitokomeza,” amesema Ndayambugwa.

Mkaguzi wa Polisi Paul Pareso ambayeni Mratibu wa Mafunzo na Mkuu wa Polisi jamii wilayani hapa ali wataka washiriki hao wa mafunzo kuhakikisha wanafuata sheria na alama za barabarani zilizopo ili kupu nguza ajali zisizo za lazima.

“Vifo vingi vinatokea kwa sababu ya uendeshaji magari na pikipiki kizembe na mwendo kasi wa madere va wasiozingatia sheria na alama hali inayosababisha watu wengi kubaki yatima, vilema na kuipa serikali mzigo wa kulea walemavu,” amesema Pareso.

Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo, Peter John kutoka Taasisi ya Grecius Driving School (GDS) alisema ulevi wa pombe imekuwa ni chanzo kikubwa cha ajali kinachoangamiza maisha ya watu wengi huku wengine wamekuwa wakiendesha vyombo hivyo vya moto kwa kutokuwa na mafunzo  na leseni ya udereva.

Baadhi ya washiriki walisema wanayo matarajio makubwa kwa elimu waliyopata kuendesha magari na pikipiki zao kwa usalama zaidi kwani wamekuwa wanatumia vyombo hivyo bila kujua sheria za usalama barabarani na kutozingatia alama zilizowekwa.

Washiriki hao walikiri kuwa wamukuwa wakiendesha vyombo hivyo kwa kupuuzia maelekezo ya polisi wa usalama barabarani hali iliyopelekea kukimbia kwa kasi pale wanapofuatiliwa na kupita vyombo vili vyo mbele yao na hatimaye kusababisha ajali vifo na watu wengi kubaki na ulemavu wa kudumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles