27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Madereva 10 wa mabasi wafungiwa miezi mitatu, kupelekwa mahakamani

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kuwafungia  kwa muda wa  miezi mitatu madereva 10 wa mabasi ambao wamekuwa wakikiuka sheria ya  usalama barabarani kwa kuendesha  kwa mwendo wa  kasi.

Pia, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabarani  kuwachukulia hatua madereva hao ikiwa ni pamoja na  kuwapeleka mahakamani kwa makosa hayo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Leo Aprili mosi 2021, Waziri Simbachawene ambaye alikuwa ameongozana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Khamisi Hamza Chilo amewataja madereva hao kuwa ni Allan Msangi ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T605 DJR  kutoka Kampuni ya Kapricon  ambalo  hufanya  safari zake katika Mikoa ya Dar es Salaam na Moshi na  hutembea kwa km 125 kwa saa .

Waziri huyo amemtaja dereva mwingine ni Hussein Dudu kutoka kampuni ya Kimotco Intertrade ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T520 CXE  ambalo hufanya safari katika Mikoa ya Arusha na Musoma na hutumia mwendokasi wa km  126 kwa saa.

Simbachawene amemtaja dereva mwingine ni Selemani Selemani ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 313 DSO kutoka kampuni ya Al Saedy  ambalo hufanya safari zake katika njia ya Dar es Salaam,Kilombero na hutumia mwendokasi wa km 103 kwa saa.

Alimtaja dereva mwingine ni Athumani Mzava ambaye huendesha gari lenye namba za usajili   T 391 kutoka kampuni ya MB Coach ambalo hufanya safari zake katika njia  ya Dar es Salaam,Arusha na hutumia mwendokasi wa km 107 kwa saa .

Waziri Simbachawene alimtaja dereva mwingine ni Juma Simba ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 340 DPW kutoka Kampuni ya Baraka Classic ambalo hufanya safari zake katika maeneo ya Dar es salaam,Masasi  na hutumia mwendokasi wa km 107 kwa saa.

Alimtaja dereva mwingine ni Salum Salum ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 121 DEA kutoka Kampuni ya Maning Nice ambalo hufanya safari zake  Dar es Salaam ,Tunduma  na hutumia mwendokasi wa  km 110 kwa saa.

Waziri Simbachawene amemtaja dereva mwingine ni Frank Masawe ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 694 DRB kutoka kampuni ya Machinga ambalo hufanya safari zake katika Mikoa ya Dar es salaam,Mtwara  na hutumia mwendokasi wa km 95 kwa saa.

Alimtaja dereva mwingine ni Innocent Thomas ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 225DTB kutoka kampuni ya Ester Luxury ambalo hufanya safari zake katika Mikoa ya Dar es salaam,Moshi  na hutumia mwendokasi wa km 107 kwa saa .

Waziri Simbachawene alimtaja dereva mwingine ni Nassib Nasoro ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 565 BED kutoka kampuni ya NBC Classic  ambalo hufanya safari zake katika Mikoa ya Tabora na Kigoma  na hutumia mwendokasi wa km 109 kwa saa.

Pia,alimtaja dereva mwingine ni  Maiko Mkindi ambaye huendesha gari lenye namba za usajili T 675 DHY kutoka kampuni ya Kilimanjaro Express ambalo hufanya safari zake katika Mikoa ya Dar es salaam na Arusha na hutumia mwendokasi wa km 100 kwa saa.

“Kwa Mamlaka niliyonayo nawafungia madereva hawa kwa muda wa miezi mitatu.Nawaagiza wamiliki wa mabasi haya ambayo madereva wamekiuka  sheria ya usalama barabarani kuhakikisha wanachukua hatua stahiki  kwa madereva wao,”amesema Waziri Simbachawene. Vilevile,ameliagiza Jeshi la Polisi kuwapeleka Mahakamani madereva hao ili iwe fundisho kwa wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles