29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 24 mbaroni kwa kuua na kuiba vitabu 500 vya shule

Na Sheila Katikula, Mwanza

Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu 24 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwamo mauaji na kuvunja ofisi za shule za msingi na kuiba vitabu.

Akielezea tukio hilo leo Alhamii Aprili mosi, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema  kwa kipindi cha miezi miwili Februari na Machi  kwa nyakati tofauti ofisi za shule tatu za msingi Wilayani Kwimba  ziligundulika kuvunjwa na vitabu 529 vya mitaala mipya vya masomo mbalimbali kuibwa.

Amesema Jeshi hilo linawashikilia walimu wa shule tatu za Msingi za Igoma, Manguluma na Bujingwa kwa kosa la kula njama za kuiba vitabu na kutengeneza matukio ya kufikirika ya kuvunja ili kufikia uhalisia wa tukio hilo.

Amesema walibaini vitabu hivyo viliibwa na kuuzwa kwa wafanyabiashara wa maduka ya vitabu jijini hapa kwani baada ya mahojiano ya kina walikili na  kuhusika na  ununuzi wa  vitabu hivyo.

“Tunawashikiria Walimu watatu ,Walinzi wanne kwa kupokea Mali  za wizi  na mtaalamu mmoja Mengi Muheta (43)ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Kishiri aliyekuwa anajihusisha na kufuta  alama za serikali inayosema kitabu hiki hakiuzwi,”amesema Muliro.

Hata hivyo ameongeza kuwa Jeshi hilo linawashikiria watu wawili kwa tuhuma za makosa ya mauaji ya mtu mmoja 42  yaliyotokea eneo la Kanyerere kata ya Mkuyuni Wilayani Nyamagana kwa kinachodaiwa wivu wa kimapenzi.

“Pembeni mwa mwili wa marehemu waliandika ujumbe kwenye sakafu uliosomeka kuwa mke wa mtu ni sumu kwani watuhumiwa wanafanyiwa mahojiano ya kina na upelelezi ukikamika watafikishwa mahakamani,”alisema Muliro.

Kamanda amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kufichua  vitendo vya uhalifu  na wahalifu  ili hatua stahiki za kisheria  zichukuliwe.

Hata hivyo amewataka wananchi kuelekea msimu wa sikukuu ya pasaka waendelee kutoa ushirikiano kwa  jeshi hilo sanjari na kuhimalisha usalama Katika mkoa huo.

“Tumejipanga   kuanzia Ijumaa kuu mpaka Jumatatu ya pasaka kuhakikisha ibada zote zinafanyika katika mazingira ya usalama kutakuwa na dori za miguu pikipiki na magari katika maeneo yote ya mjini na visiwani kutakuwa salama,”amesema Muliro

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles