24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maandalizi ya Fury na Klitschko yapamba moto

Tyson FuryLONDON, ENGLAND

KAKA wa bondia wa uzito wa juu duniani, Tyson Fury, Peter Fury, amethibitisha mchezo wa marudio wa uzito wa juu unaomhusu mdogo wake dhidi ya Wladimir Klitschko, unatarajiwa kutangazwa rasmi muda wowote ili uweze kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Fury na Klitschko wanatarajiwa kupambana kwa mara ya pili mfululizo kutokana na matokeo ya awali kuwa na ukakasi.

Mchezo huo wa marudio uliotakiwa kufanyika Julai 9 mwaka huu, uliahirishwa baada ya Fury kupata matatizo ya kifundo cha mguu Juni mwaka huu.

Hata hivyo, Fury na kaka yake Juni 24 mwaka huu, walituhumiwa kutumia dawa za kuongeza nguvu ambapo hawakukana tuhuma hizo.

Peter alibainisha kupitia ukurasa wake wa  Twitter kwamba, licha ya kupita katika vizingiti vingi vya kisiasa, pambano la mdogo wake huenda likakamilika na kutangazwa muda mfupi ujao.

“Nafikiri tupo katika hatua ya mwisho ya maandalizi ya pambano hilo, tunatarajia wahusika watatangaza muda mfupi ujao ili  Oktoba 29 mwaka huu tupate burudani ulingo wa Manchester Arena,” alisema Peter.

Fury aliongeza kuwa ulingo wa Manchester Arena uliandaliwa kabla kwa ajili ya pambano hilo, wanasheria na mapromota wapo tayari kwa mchezo huo.

Bondia huyo Mwingereza Novemba mwaka jana, alitikisa dunia kwa kufanikiwa kunyakua mkanda wa WBA (Super), IBF, WBO na IBO wa uzito wa juu wa dunia dhidi ya Dusseldorf.

Ulingo wa Manchester Arena pia ulitumiwa hivi karibuni kugombea mkanda wa IBF na bondia  Anthony Joshua ambaye alishinda mkanda huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles