27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Maalim Seif atoa masharti kwa CCM

Na Mwandishi Maalum, Marekani

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ametoa masharti ambayo yakifuatwa chama hicho kitakuwa tayari kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutafuta suluhu ya mgogoro wa siasa visiwani humo.

Alikuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na   Taasisi ya International Republican Institute (IRI) mjini Washington DC,   Marekani juzi.

Maalim Seif alisema:  “Tuko tayari kushirikiana na Serikali ya CCM visiwani Zanzibar kwa kuunda Serikali ya mpito ya Umoja wa kitaifa itakayooongoza kwa muda.”

“Baada ya hapo tutakuwa tayari kwenda kushiriki uchaguzi mpya kwa sharti tu usimamiwe na chombo huru cha kimataifa”.

Seif alisema hayo wakati akieleza hali ya siasa visiwani humo pamoja na matukio yaliyopelekea hali hiyo.

Licha ya ukandamizaji huo kutoka serikali na vyombo vya dola, alieleza jinsi chama chake kinavyoendesha kampeni ya upinzani kwa njia ya amani bila kuhusisha machafuko.

Seif alisisitiza kwamba Zanzibar haiwezi kuendeshwa kwa staili ya biashara kama kawaida.

Alitahadharisha kwamba bila hatua kuchukuliwa kuokoa hali mbaya ya siasa visiwani humo, kuna uwezekano mkubwa Zanzibar kugeuka kuwa maficho ya Waislamu wenye itikadi kali.

“Hofu yetu ni kwamba kwa kadiri ya njia za demokrasia zinapoendelea kufungwa, makundi ya dini ya msimamo mkali yatapata nafasi.

“Zanzibar kwa muda mrefu ina uhusiano na kambi zinazohusiana na harakati za wanamgambo wa Kiislamu kama vile Somalia, sehemu za Pwani ya Mashariki ya Kenya na hata Mashariki ya Kati.

“Kinachotokea Zanzibar ni mfano wa visababishi kwa jamii kuchagua kuangukia katika machafuko ya itikadi kali, utawala dhaifu wa uchumi; umasikini na ukosefu wa ajira, hasa miongoni mwa vijana. Yote yakisababishwa na hali ya kukata tamaa, ukosefu wa haki na ukandamizaji na ukosefu wa uhuru wa siasa,” alisema na kuongeza:

“Ndiyo maana tunakataa kukata tamaa na ndiyo maana harakati zetu za demokrasia ni zaidi ya Zanzibar.

‘Sisi ni nchi ndogo, lakini kinachotutokea kina athari mbaya na pana kwa bara Afrika na duniani kwa ujumla– iwe kwa namna nzuri kama kichocheo cha maendeleo ya uchumi katika eneo hili au namna mbaya kuwa ukandamizaji unakigeuza kisiwa chetu kiwe mwathirika wa makundi yenye itikadi kali za dini”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles