24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MA-DC WAWILI KIKAANGONI

KASANDRA HASSAN (TUDARCO) Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, imezitaka mamlaka za uteuzi wa viongozi wa umma kusimamia maadili ya viongozi hao ili madaraka yasiwe chombo cha kuvunja sheria.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nyanduga alipozungumza na MTANZANIA kuhusu tuhuma zinazowakabili wakuu wawili wa wilaya za Chemba, mkoani Dodoma na Hai mkoani Kilimanjaro.

Akizungumzia tukio la Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa, kudaiwa kumweka mahabusu  mwalimu Erasto Mhagama wa Shule ya Sekondari Lerai, Nyanduga alisema suala hilo linatakiwa kuendelea kufuatiliwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwa aliyewekwa ndani ni mwalimu.

“Suala hilo kwa sasa linalifuatiliwa na CWT na  wameahidi kuchukua hatua, hivyo ni vema tuwaache weendelee nalo na watakapofika mwisho, ndipo tume inaweza kutoa tamko.

“Kimsingi, taasisi zote za Serikali zinapaswa kufanya kazi kwa kujitegemea badala ya kuingiliana, hebu tusubiri CWT waendelee na hatua walizosema wanazichukua.

“Lakini, matukio ya wakuu hao wa wilaya yanaangukia katika matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi wa umma.

“Pamoja na uwapo wa matukio hayo, tumewahi kuongelea matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi wa umma wakiwamo Ma-DC na wanalifahamu hilo.

“Kwa hiyo, mamlaka zinazoteua viongozi wa umma, zinapaswa kurejea na kusimamia maadili kwa viongozi wake ili kuhakikisha madaraka siyo chombo cha ‘kuabuse’ sheria,” alisema Nyanduga.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Joseph Ishengoma aliiambia MTANZANIA, kuwa matukio yaliyofanywa na wakuu  wa wilaya, waliyajua kupitia vyombo vya habari.

Kutokana na hali hiyo, alisema bado wanaendelea kuyachunguza kwa kutumia sheria namba 13 ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.

“Sheria hii ipo na inaipa mamlaka sekretarieti kuanzisha uchunguzi dhidi ya jambo lolote linaloifikia likimlalamikia kiongozi wa umma.

“Ikiwa kiongozi wa umma amevunja sheria ya maadili ya uongozi, hatua ambazo huwa zinapendekezwa ni za kiutawala. Kwa hiyo, hatuwezi kuwahukumu hadi hatua za uchunguzi zitakapofuatwa,” alisema Ishengoma.

Wakati huo huo, Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Kilimanjaro, kimepeleka barua ya malalamiko kwa Mkuu wa Mkoa huo, Anna Mgwhira, kumlalamikia Byakanwa juu ya kitendo alichomfanyia mwalimu Mhagama.

Malalamiko hayo, yaliwasilishwa jana na  Katibu wa CWT Mkoa wa Kilimanjaro, Digna Nyaki.

Akizungumza kwa ufupi na waandishi wa habari, Nyaki alisema chama chake kimeeleza kwa kina tuhuma zinazomkabili mkuu huyo wa wilaya.

“Hatua tuliyofikia kwa sasa ni nzuri, tumefikishia malalamiko mkuu wetu wa mkoa, juu ya udhalilishaji uliofanywa na DC wa Hai.

“Katika hili, lengo letu ni kuhakikisha walimu wote wanaheshimiwa na siyo kudhalilishwa kama alivyofanya mkuu huyo wa wilaya.

“Kwa kifupi, baada ya kumkabidhi barua mkuu wa mkoa, aliahidi kuyafanyia kazi malalamiko yetu. Lakini, msimamo wetu lazima DC aombe radhi ndani ya siku 30 na kama atakaidi hilo, basi ajue tutamfikisha mahakamani.

“Tunaamini mkuu wa mkoa atalifanyia kazi suala hili kwa sababu udhalilishaji aliofanyiwa mwalimu mwenzetu, umejeruhi mioyo ya walimu mkoani hapa,” alisema Nyaki.

Hata hivyo, Mghwira alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alikataa kufanya hivyo kupitia kwa msaidizi wake aliyetajwa kwa jina la Daniel Mchomvu, kwamba anakabiliwa na majukumu mengi ya kikazi.

BUNDA

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili ameliagiza Jeshi la Polisi  kukamatwa kwa Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) na wenzake kwa madai ya kuhamasisha wananchi kutoutambua uongozi wake na uchochezi.

Wabunge wengine ni Esther Matiko (Tarime Mjini),John Heche (Tarime Vijijini), Joyce Sokombi (Viti Maalumu Mkoa wa Mara) na Naibu Katibu Mkuu wa Zanzibar, Salumu Mwalim.

Wengine ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche, Katibu wa Jimbo la Bunda Mjini, Daniel  Ayot, madiwani Georgies  Miyawa (Kata ya Nyamakokoto), Joash Kunaga (Kata ya Bunda Mjini), Mwamba Wasira (Kata ya Nyasura) na makada mengine ambao majina yao hayakupatikana mara moja.

alipozungumza na MTANZANIA kuhusu tuhuma zinazowakabili wakuu wawili wa wilaya za Chemba, mkoani Dodoma na Hai mkoani Kilimanjaro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles