30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

SUMAYE: MAHAKAMA IMEWEKWA KITANZINI

Na JUSTIN DAMIAN

-DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Frederick Sumaye, amesema kitendo cha mamlaka za juu za nchi kuingilia uhuru wa mahakama ni wazi mhimili huo umewekwa kitanzini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu hatua ya Serikali kumnyang’anya mashamba, Sumaye alisema ni wazi kwa sasa misingi ya utawala bora imepewa kisogo.

Sumaye alisema baada ya kunyang’anywa mashamba yake mawili ambayo yanamilikiwa na familia yake kihalali moja lilipo Mabwepande  Dar es Salaam lenye ukubwa wa ekari 33 na jingine la Morogoro lenye ukubwa wa ekari 326, awali kabla ya kuwepo kwa mchango huo alikwenda kufungua kesi mahakama kuzuia mipango hiyo.

“Baada ya matukio hayo, tulifungua kesi mbili Mahakama Kuu kwa kufuata taratibu zote za kisheria, moja dhidi ya wavamizi na nyingine dhidi ya serikali. Kesi ziko mahakamani zinaendelea, mahakama imeweka zuio la muda kwa shughuli yoyote kutoendelea katika eneo hilo na wahusika wote yaani wavamizi na serikali wana habari na hatua hizo za mahakama.

 

“Leo (jana) tunavyoongea shamba hilo limetwaliwa na Rais tena kwa maagizo yaleyale ya kusema ligawanywe kwa wananchi na wale wavamizi wapewe kipaumbele kama alivyowatangazia Mkuu wa Wilaya Ally Hapi hapo nyuma,” alisema.

 

Sumaye alisema kuwa tangu utawala wa awamu ya tano uingie madarakani, misingi ya utawala bora umeanza kuwa bora imekuwa ikipindwa ikiwemo uwepo wa matumizi ya nguvu yanayofanywa na vyombo vya dola.

 

“Katika awamu hii kwa mara ya kwanza tumeshuhudia Jeshi la Polisi lenye silaha likiingizwa ndani ya Bunge kuwapiga na kuwatoa nje wabunge wasio na silaha, wanaobishana bungeni kwa kwa sababu ndiyo kazi yao ya msingi kupingana kwa hoja.

 

“Si mara ya kwanza wabunge   wa   upande mmoja kutokukubaliana na upande mwingine au hata na Spika na katika hali ya namna hiyo huahirisha Bunge ili vyama vikae katika “Caucus” zao kutulizana hasira na busara ichukue nafasi yake badala ya hasira.

 

“Hali ya namna hii huikumba mabunge mengi sana duniani wengine hata kufikia hatua ya wabunge kuchapana makonde lakini huoni jeshi la nje likiingizwa bungeni maana Bunge lina askari wake.

 

“Kilichotokea kwetu ni, kwanza, mhimili wa utawala umeingilia mhimili wa kutunga sheria yaani Bunge na pili kuwatisha wabunge ili waogope kuikosoa serikali jambo ambalo ni wajibu wao wa msingi na kwa kiasi kikubwa serikali imefanikiwa sana katika hili,” alisema Sumaye

 

Licha ya hali hiyo alisema mara kadhaa mali za watu zimekuwa zikitwaliwa na serikali bila kufuata sheria na wakati mwingine kesi za pingamizi zikiwa mahakamani.

 

“Nyumba za watu zinavunjwa hata kama kesi ziko mahakamani na pengine nyumba zenye hati ya serikali hiyo hiyo. Mashamba na viwanda vinachukuliwa bila kufuata taratibu za sheria. Sipingi Serikali kuchukua mali ya raia au kuvunja nyumba ya raia lakini taratibu za sheria lazima zifuatwe,” alisema

 

Akizungumzia shamba la Mabwepande  alisema linamilikiwa kihalali na mwanaye aliyemtaja kwa jina la Franklin Frederick aliyelinunua mwaka 1999.

 

Alisema tangu wakati huo wamekuwa wakilima mazao mbalimbali shambani hapo.

 

“Wakati  tunapanga  mipango  hii,  Septemba  mwaka  2015  wakati  wa  kampeni shamba hili na mashamba mengine tena mengine ya viongozi wa CCM yalivamiwa na wavamizi. Tulipeleka taarifa sehemu zinazohusika kwa maana ya polisi Wazo na serikali ya kijiji lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kuwaondoa wavamizi wetu.

 

“Lakini wavamizi katika yale mashamba mengine waliondolewa haraka kwa nguvu ya Jeshi la Polisi  na  maeneo yale ambayo  mengine labda yalikuwa hayajawahi  kutumika kwa shughuli zozote yakawa salama. Tulifanya kila juhudi ili wavamizi waondolewe lakini kila juhudi ziligonga ukuta,” alisema

 

Kutokana na hali hiyo alisema kumuona IGP wa wakati huo Ernest Mangu sambamba na kumwandikia barua akihitaji msaada wake au aruhusiwe awatoe mwenyewe wavamizi hao.

Alisema alitakiwa na Mangu kuafuata sheria sambamba na kwenfa kuuona aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maaluya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro, ambaye alimwagiza RPC wa Kinondoni huku akiambiwa kuwa suala la shamba lake liachwe kama lilivyo kwa sababu lina maagizo kutoka juu.

 

Akizungumzia shamba la o linamilikiwa na mke wake mama Esther Sumaye ambaye alilinunua kuotoka kwa Chama cha Ushirika kinachojulikana  cha Morogoro Farmers Primary Cooperative Society mwaka 2002 huku akikisitiza kuwa kumekuwa na upotoshaji kuwa shamba hilo ni mali ya kijiji.

 

“Mwanzoni mwa mwaka jana, 2016, Rais alipita maeneo ya Mvomero na kuagiza kuwa mashamba yote ambayo hayajaendelezwa apelekewe orodha ayafute. Baraza la madiwani walikaa kupitia orodha hiyo na shamba la Esther Sumaye halikuwa mojawapo ya mashamba yaliyopelekwa,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles