27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA: NI AIBU WANANCHI KUKOSA MAJI SAFI

WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.

Na MWANDISHI WETU-TABORA

WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amesema ni aibu kufikisha miaka 50 tangu kupata Uhuru lakini bado wananchi wanakosa huduma ya maji safi.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana alipotembelea Kata ya Tumbi na kufanya uzinduzi wa msingi wa Chadema na kufanya kikao cha ndani na wanachama, wadau na wananchi.

Wakati akiendelea kuzungumza na wananchi hao waliojitokeza kwa wingi walilalamikia tatizo la ukosefu wa maji mkoani hapo.

“Watanzania wengi hawana maji na ni jambo la aibu hasa ukizingatia tuna miaka zaidi ya 50 baada ya kupata uhuru, wananchi wetu wengi bado hawana maji, nyinyi mna maji hapa?” alihoji Lowassa na wananchi kwa umoja wao kujibu hakuna.

Pia Lowassa alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa Tumbi na Tabora kwa kumpigia kura kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

Wananchi hao walipongeza uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema wa kuamua kushuka hadi ngazi za chini za uongozi na kuzungumza nao pamoja na kupanga mikakati ya jinsi gani wanaweza kukijenga chama hicho kuwa imara zaidi hasa baada ya kutoka katika uchaguzi kulileta hamasa kubwa kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles