27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA, MAALIM SEIF, KINGUNGE WAJIFUNGIA KUTWA NZIMA KUJADILI UKAWA

lowasseif

Na Mwandishi Wetu

-DAR ES SALAAM

VIONGOZI wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, wamejifungia kujadili hali ya kisiasa nchini pamoja na hatima ya umoja huo.

Mbali na Lowassa, viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika jana Dar es Salaam, ofisini kwa waziri mkuu huyo wa zamani, ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru.

Mbali na vigogo hao, pia walikuwapo Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Juju Danda na Naibu Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni kiongozi wa wabunge wa CUF, Riziki Shaali Mngwali.

Chanzo cha kuamika kiliiambia MTANZANIA kuwa pamoja na mambo mengine, viongozi hao walijadili kwa kina hatima ya Ukawa, hasa kutokana na kile kilichoelezwa vurugu zinazofanywa na Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake linalomuunga mkono.

“Ni kweli tangu saa 8 mchana viongozi wamekutana ofisini kwa Lowassa Mikocheni kujadili hatima ya Ukawa na vurugu ndani ya CUF.

“Na pia wamebadilishana taarifa juu ya hali ya kisiasa nchini na jinsi ya kushiriki katika uchaguzi wa marudio katika Jimbo la Dimani, Zanzibar na madiwani katika kata zaidi ya 20, ambao unatarajiwa kufanyika Januari 22, 2017,” kilisema chanzo hicho.

MTANZANIA ilipomtafuta Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa Umma wa CUF, Mbarara Maharagande, alithibitisha kukutana kwa viongozi hao, ingawa hakutaka kueleza kwa ndani kilichojadiliwa.

“Ni kweli viongozi wamekutana. Ukiachia Lowassa na Maalim Seif, wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF Taifa, Julius Mtatiro, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Katibu Mkuu NCCR-Mageuzi, Juju Danda na Balozi Musinga Bandora.

“Sasa kilichojadiliwa ni masuala ya uchaguzi na pia hali ya kisiasa nchini,” alisema kwa kifupi Maharagande.

Pamoja na ufafanuzi huo, MTANZANIA lilimtafuta mmoja wa wasaidizi wa Lowassa ili kujua kwa kina viongozi hao wametoka na uamuzi gani, ambaye alisema kuwa kikubwa ni suala la uchaguzi na hali ya mshikamano ndani ya Ukawa.

“Unajua vurugu zimekuwa zikifanywa ndani ya CUF kama sehemu ya Ukawa, lakini pia kama sehemu ya umoja ni lazima viongozi wakutane na kujadiliana kwa kina. Ingawa huenda wakatoka na uamuzi mzito juu ya yanayoendelea ndani ya CUF,” alisema msaidizi huyo wa Lowassa ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini.

Viongozi hao wamekuwa wakikutana kujadiliana masuala kadhaa, ikiwamo kutoa matamko ya pamoja kuhusu ya hali ya kisiasa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles