Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ametruma salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kutokana na ajali ya Kivuko cha MV Nyerere, kilichozama jana Ukerewe, jijini Mwanza.
Ajali hiyo ilitokea jana wakati kivuko hicho kikitoka Bugorora (Ukerewe) kwenda Bwisya (Ukara) kikiwa na abiria ambao idadi yao inahofiwa kuwa zaidi ya 100 ambapo hadi sasa watu zaidi ya 90 wanahofiwa kufariki dunia katika ajali hiyo.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea jana Septemba 20, huko Ukerewe mkoani Mwanza.
“Nawapa pole ndugu wa wote waliopoteza maisha, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na watanzania wote kwa ujumla,” amesema Lowassa.
Lowassa amesema huo ni msiba wa nchi nzima kwani maisha ya wananchi wengi namna hiyo yanapopotea kwa ajali, ni lazima tujiulize na kujipanga kama taifa ili yasitokee tena.
Pole kwetu wote ,nikweli kwamba serekali imeshindwa simamisha matukio ya namna hii ambayo yanaweza kuzuilika kwaku hakikisha RAIA tunakuwa katika usalama wa uhakika?