26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

LOWASSA APONGEZA USHINDI WA TRUMP

Na JANETH MUSHI, ARUSHA


lowassaWAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewapongeza raia wa Marekani kwa kumchagua Donald Trump kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Lowassa, Trump atakuwa rais mwenye kufanya uamuzi mgumu kwa kuwa ni shupavu na ana uwezo.

Trump ambaye ni Rais Mteule wa Marekani, alichaguliwa kuwa Rais mpya wa Marekani baada ya kumshinda mpinzani wake, Hillary Clinton, mwishoni mwa mwaka jana.

Lowassa aliyasema hayo jana katika misa maalumu ya shukrani ya mwaka mpya 2017 iliyoshirikisha madhehebu mawili ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli na Kanisa Katoliki, wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha.

Ibada hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo wa Serikali na wa vyama vya siasa, wakiwamo Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ambaye pia ni Katibu wa Chadema, Mkoa wa Arusha.

“Wamarekani hawakufanya makosa kumchagua Trump kwani anaonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza Taifa hilo tajiri duniani ambalo linategemewa na mataifa mengine.

“Dunia imebadilika, amechaguliwa rais mmoja huko Marekani ambaye ni mwamba kweli kweli.

“Hatuwezi kumtabiri mambo yake yatakavyokuwa, lakini inabidi kila mtu afanye kazi kwa bidii na kwa maarifa kwa sababu huyo hakubali upuuzi wowote,”alisema Lowassa.

Lowassa ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Monduli kwa miaka 20, aliwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuacha kulalamika kwani hiyo ndiyo njia iliyo sahihi ya kuweza kuondokana na umasikini.

“Mwaka jana, tarehe kama hii, tulimuaga Mbunge Julius Kalanga na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isack Joseph, nikawaambia nawatakia heri wachape kazi vizuri, naona wamefanya vizuri au siyo?alihoji Lowassa.

Akizungumzia upande wake, Lowassa alisema hivi sasa anafanya siasa za kimataifa tofauti na siasa alizokuwa akifanya kipindi kilichopita.

“Mimi sitaki kusema sana maana watasema napiga siasa. Siku hizi napiga siasa za kimataifa, naomba niwatakie heri ya mwaka mpya na kila mtakachoshika, Mungu akibariki kiwe dhahabu,”alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles