25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Lori laua watembea kwa miguu wanne

roads_lorry

NA PENDO FUNDISHA, MBEYA

WATU wanne, wamepoteza maisha papo hapo na wengine 22 kujeruhiwa baada ya kugongwa na lori barabarani.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, Zahiri Kidavashari , aliwaambia waandishi wa habari jana, kwamba lori hilo lilikatika breki lilipokuwa kwenye mtelemko eneo la Mbalizi na kwamba lilikuwa limebeba mifuko ya saruji.

“Ajali hiyo ilitokea juzi, saa mbili usiku ikihusisha lori lenye namba za usajiri T 215 CLB lililokuwa na tela lenye namba T 876 CLB na lilikuwa likitokea mjini Mbeya likielekea Sumbawanga.

“Kabla ya ajali, lori hilo lilifeli breki na kupoteza mwelekeo kutokana na mwendo kasi ambapo dereva alishindwa kulimudu na kusababisha liparamie magari mengine manne na watembea kwa miguu.

“Kwa bahati mbaya, hadi sasa watu watatu waliofariki bado hawajafahamika ila mmoja aliyefahamika kwa jina la Philipo Cheyo, alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya. Ile miili ya watu watatu, imehifadhiwa katika Hospitali ya Ifisi.

“Yale magari yaliyogongwa ni yenye namba za usajili T 705 CVK Toyota Coaster, T 720 CFH ainaya pajero na toyota canter lenye namba za usajiri T 719 DEH,” alisema Kamanda Kidavashari.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali Teule ya Mbalizi Ifisi, Elimati Sanga, alikiri kupokea majeruhi 22 na kusema watano kati yao waliokuwa na hali mbaya, walihamishiwa katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya.

Kuhusu majeruhi waliolazwa hospitalini hapo, alisema wanaendelea vizuri.

Katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya, Lucy Elias aliyekuwa muuguzi wa zamu alikiri kupokea majeruhi 10 wakiwamo waliopewa rufaa kutoka Hospitali ya Ifisi.

Baadhi ya majeruhi waliokuwa kwenye Coaster waliiambia MTANZANIA, kwamba gari lao liligongwa na lori kwa kuwa dereva wao alisimama eneo lisiloruhusiwa kisheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles