29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rose Ndauka: Ati nini, ulabu unanipa mzuka?

Rose Ndauka
Rose Ndauka

NA JOHANES RESPICHIUS,

YAPO madai ya chini kwa chini kwamba eti staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka ili aweze kuigiza kwa uhalisia sawasawa lazima apige ulabu location, jambo ambalo amelikanusha vikali.

Akizungumza na Juma3tata kwa njia ya simu juzi Jumamosi, Rose alisema kuwa hajawahi kunywa pombe location na kwamba maneno hayo yapuuzwe kabisa na mashabiki wake.

“Nani kasema maneno hayo? Yaani nitafute hisia za kuigiza vizuri kwa kunywa pombe? Siyo kweli kabisa,” alisema Rose.

Alipoulizwa anatumia stata gani ili kumfanya awe bora awapo nyuma ya kamera alijibu: “Mungu tu. Kabla sijaanza kurekodi, lazima nisali kimyakimya tena nikiwa peke yangu, ndipo naingia mzigoni na kazi inayotoka hapo nadhani mwenyewe unajua.”

Inaelezwa kuwa baadhi ya wasanii wa filamu hutumia vilevi mbalimbali kabla ya kuanza kuigiza ili kuwapa stimu na kuwaondolea uoga wakati wakiigiza.

Hata kwa upande wa wasanii wa Bongo Fleva, yapo madai kuwa baadhi yao hawapandi jukwaani kupiga shoo kabla ya kupiga vitu vikali vikiwemo pombe au mihadarati aina ya bangi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles