27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

LIVERPOOL YAIKATALIA BARCELONA OFA YA TATU

LIVERPOOL, ENGLAND

UONGOZI wa klabu ya Liverpool, umekataa ofa ya tatu kutoka kwa matajiri wa klabu ya Barcelona juu ya kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Philippe Coutinho, raia wa Brazil.

Klabu hiyo ya Merseyside, wameweka wazi kuwa hawana mpango wa kumuacha mchezaji wao huyo akiondoka katika kipindi hiki cha majira ya joto.

Awali Barcelona waliweka mezani kitita cha pauni milioni 72 ili kumsajili mchezaji huyo, lakini Liverpool wakaikataa ofa hiyo, wakaja tena na pauni milioni 80 bado Liverpool ikaendelea na msimamo wake kuwa mchezaji huyo hauzwi, mapema wiki hii Barcelona waliongeza kitita cha fedha na kufikia pauni milioni 90, lakini kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesisitiza mchezaji wake hauzwi.

Coutinho mwenyewe mwenye umri wa miaka 25, anaonekana kuwa na nia ya kutaka kuondoka katika kipindi hiki cha usajili na anahusishwa kutaka kumfuata rafiki yake wa karibu Neymar katika klabu ya PSG.

Awali Neymar alitajwa kuwa miongoni mwa watu wa karibu ambao wanamshawishi Coutinho kujiunga na klabu ya Barcelona, lakini baada ya Neymar kutimkia klabu ya PSG inadaiwa anamshawishi aungane naye katika klabu hiyo ya matajiri wa mjini Paris.

Uongozi wa Barcelona umeweka wazi kuwa una imani ya kumsajili mchezaji huyo katika kipindi hiki cha uhamisho japokuwa Liverpool hawataki kumuacha akiondoka.

Liverpool inatarajia kushuka dimbani kesho katika mchezo wao wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi Kuu nchini England dhidi ya Watford, lakini kiungo wao huyo mshambuliaji ataukosa mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na maumivu.

Coutinho alishindwa kumaliza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake juzi kutokana na kusumbuliwa na maumivu, lakini kuna uwezekano akawa fiti kwenye mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu wiki ijayo.

Kocha wa Liverpool, Klopp, ameweka wazi kuwa kikosi chake msimu huu ni kipana na anatarajia kufanya makubwa katika ushindani wa ligi.

“Msimu uliopita tulimaliza nafasi ya nne, kila mmoja alikuwa na furaha kwa hatua hiyo, ni wazi kwamba yalikuwa matokeo mazuri kwetu kutokana na juhudi zetu, msimu huu tunatarajia kufanya makubwa zaidi, tunaamini tunaweza kufanya hivyo kutokana na ubora wa kikosi chetu,” alisema Klopp.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles