22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

PAZIA LA LIGI KUU ENGLAND KUFUNGULIWA LEO

LONDON, ENGLAND

HATIMAYE pazia la michuano ya Ligi Kuu nchini England msimu wa 2017/2018, linatarajiwa kufunguliwa leo kwenye uwanja wa Emirates, huku wenyeji wa uwanja huo, Arsenal wakiwakaribisha wapinzani wao Leicester City.

Ni mchezo wa pekee ambao utapigwa leo hii, michezo mingine ikitarajiwa kupigwa kesho kwenye viwanja mbalimbali.

Arsenal wanashuka dimbani huku wakiwa tayari wametwaa taji la Ngao ya Jamii baada ya kuwachapa wapinzani wao mabingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita, Chelsea mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalti kutokana na dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1.

Msimu uliopita Arsenal walifanya vibaya kwa mara ya kwanza kwenye msimamo wa ligi wakishika nafasi ya tano kwa mara ya kwanza kwa miaka 20, hivyo kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger, atahakikisha anafanya vizuri msimu huu.

Wachezaji ambao wataukosa mchezo wa leo kutokana na kuwa majeruhi ni pamoja na Alexis Sanchez, ambaye anasumbuliwa na tumbo, Aaron Ramsey, Mesut Ozil na Per Mertesacker ni majeruhi, hivyo wanaweza kuukosa mchezo huo wa ufunguzi. Wakati huo, Laurent Koscielny, ataukosa mchezo huo kutokana na kuitumikia kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo wa mwisho msimu uliopita dhidi ya Everton.

Kwa upande wa Leicester City ikiwa chini ya kocha wao mpya, Craig Shakespeare, ameweka wazi kuwa atahakikisha anawatumia wachezaji wake wapya aliowasajili msimu huu ikiwa ni pamoja na Kelechi Iheanacho, Harry Maguire, Vicente Iborra na Eldin Jakupovic.

Mambo ya kukumbuka katika michezo ya ufunguzi wa ligi ni kwamba, Arsenal wamefanikiwa kushinda kila mchezo katika 10 waliokutana na Leicester kwenye uwanja wa Emirates, lakini Arsenal wameshinda mchezo mmoja tu kati ya saba ya ufunguzi wa ligi na wamefungwa mitatu kati ya minne iliyopita.

Katika mchezo wa ufunguzi wachezaji wengi wa Arsenal wamekuwa wakioneshwa kadi nyekundu nyingi kuliko timu yoyote ya Ligi Kuu England.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles