30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

NIYONZIMA ALIKOROGA KWA MASHABIKI RWANDA

Na ZAINAB IDDY- DAR ES SALAAM

IMEBAINIKA kuwa hatua ya kiungo wa zamani wa Yanga, Haruna Niyonzima, kuachana na timu hiyo na kujiunga na Simba kimewakera baadhi ya mashabiki nchini Rwanda.

Niyonzima amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kushindwa kuafikiana na Yanga kuhusu dau la kusaini mkataba mpya baada ya ule wa awali kumalizika msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba ilimtambulisha rasmi kiungo huyo raia wa Rwanda katika tamasha maalumu la siku ya klabu hiyo ‘Simba Day’ lililofanyika Jumanne ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika tamasha hilo, kikosi cha Simba kilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo wa timu hiyo, Mohamed Ibrahim ‘Mo’.

Akizungumza na MTANZANIA, Kocha Msaidizi wa Rayon Sport ya Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’, alisema tangu kuanza fununu za Niyonzima kujiunga na Simba mashabiki wa soka nchini Rwanda walionekana kutomuunga mkono, waliamini hatua hiyo ingethibitisha madai ya siku nyingi kwamba ni mnazi wa Wekundu hao.

“Kwa Rwanda wadau wengi wa mpira hawakufurahia kitendo cha yeye kutoka Yanga kwenda Simba, kwani imethibitisha kwamba zile tuhuma za kudaiwa ni mnazi wa timu hiyo zilikuwa na ukweli.

“Ukiwasikiliza wengi wanasema ni bora angeenda timu nyingine yoyote Tanzania kuliko Simba ambao ni wapinzani wa asili wa Yanga huku wakifanyiana vitendo vya kutaka kuporomoshana kisoka,” alisema.

“Aliporejea nyumbani Rwanda alikutana na mashabiki na kuwaeleza ukweli sababu za kujiunga na Simba kuwa ni fedha na kwamba yeye  yupo Tanzania kikazi jambo ambalo hakuna aliyekubaliana nalo, lakini kwa kuwa ni uamuzi wake hakuna namna zaidi ya kumuacha afanye kazi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles