31.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Liverpool wataendeleza ubabe wao England?

Liverpool, England

BAADA ya mapumziko ya wiki mbili, michuano ya Ligi Kuu nchini England inatarajia kuendelea leo kwa michezo saba kupigwa kwenye viwanja mbalimbali.

Hii ni michezo ya tano inayoanza kupigwa leo, Liverpool wamekuwa vinara wa ligi hiyo baada ya kushinda michezo yote minne ya awali.

Leo watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani wakiwakaribisha wapinzani wao Newcastle United ambayo imeanza vibaya msimu huu kwa kufungwa michezo miwili,  kushinda mmoja na sare mmoja, hivyo kuwafanya washike nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi nne.

Historia inawabeba Liverpool, leo itakuwa mara ya 153 kwa timu hizi kukutana kwenye michuano mbalimbali, kati ya 152 walizokutana Liverpool wamekuwa wababe wakishinda mara 72, wakati huo Newcastle United ikishinda mara 42 na kutoka sare mara 38.

Lakini kwa mchezo huo wa leo Liverpool wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na ubora wao hasa kwa misimu hii miwili.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa Mei mwaka huu huku Newcastle wakiwa nyumbani walikubali kichapo cha mabao 3-2, lakini soka ni mchezo wa makosa na chochote kinaweza kutokea.

Mchezo mwingine wa leo ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Manchester City ambao watakuwa ugenini kukutana na Norwich ambao wamepanda daraja msimu huu.

Kwenye msimamo wa ligi Manchester City inashika nafasi ya pili baada ya kutoa sare mchezo mmoja dhidi ya Tottenham kwenye uwanja wa nyumbani Etihad.

Kwenye mchezo wa leo unaweza ukawa mgumu kwa Manchester City kutokana na kuwa na wachezaji wengi majeruhi katika safu ya ulinzi, lakini kutokana na ukubwa wa kikosi chao wanaweza kufanya lolote kwa kuwategemea viungo wakabaji.

Kwa upande mwingine Manchester United watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani wakipambana na Leicester City. Huu ni mchezo ambao unasubiriwa sana na mashabiki huku wakiamini Leicester inaweza kuwatunishia misuri wapinzani hao kutokana na kuanza vizuri msimu huu.

Leicester wamefanikiwa kushinda michezo yao miwili ya awali huku wakipoteza miwili, hivyo kuwafanya washike nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, wakati huo United chini ya kocha wao Ole Gunnar Solskjaer wakishinda mchezo mmoja, sare mara mbili na kichap mchezo mmoja.

Michezo mingine ya leo ni pamoja na Brighton dhidi ya Burnley, Tottenham dhidi ya Crystal Palace, huku Chelsea wakiwa ugenini kupambana na Wolves, wakati huo Sheffield wakiwakaribisha Southampton.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles