23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Simba inawachapa

Theresia Gasper,Dar es salaam

MSHAMBULIAJI Meddie Kagere ameendelea kutakata, baada ya jana kuifungia Simba bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kagere tayari amefunga mabao mawili msimu huu, baada ya kuifungia Simba bao pekee ilipoitandika JKT Tanzania mabao 3-1, katika  mchezo wa kwanza uliopigwa pia kwenye uwanja huo.

Kipindi cha kwanza kilimalizika Simba na Simba kwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa, baada ya kufungana bao 1-1.

Kagere alifunga bao la kuongoza la Simba dakika ya 18, baada ya  kumalizika mpira uliopigwa na Sharaf Shiboub.

Lakini  shangwe za mashabiki wa Simba hazikudumu muda mrefu kwani Riphat Msuya aliisawazishia Mtibwa Sugar kwa kufunga bao dakika ya 21, akiunganisha kona iliyochongwa na Issa Rashid  maarufu Baba Ubaya.

Kipindi cha pili, kila upande ulizidisha kasi ya mashambulizi kwa lengo la kusaka mabao zaidi.

Dakika ya 63, Kocha wa Simba, Patrick Auusems alimtoa Hassan Dilunga na kumwingiza Miraj Athuman kabla ya Kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila kumtoa Haruna Chanongo dakika ya 67 na kumwingiza Omar Hassan.

Dakika ya 68, Miraj aliiandikia Simba bao la pili kwa shuti kali, baada ya kuunganisha pande la Shiboub.

Dakika ya 79, Aussems alimtoa Clatous Chama na kumwingiza Fransis Kahata.

Mtibwa ikamtoa Ismail Mhesa dakika ya 81 na kuingia Abdul Haule kabla ya Rashid kutoka dakika ya 85 na kuingia Henry Joseph.
Dakika ya 89 alitoka Shoboub na kuingia Jonas Mkude.

Pamoja na mabadiliko ya kila upande, dakika 90 zilikamilika kwa Simba kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, wenyeji Costal Union waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC.

Mabao ya Coast yalifungwa na Shabaan Idd dakika ya 62 na Ayub Lyanga dakika ya 75.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles