TIMU za Manchester United na Liverpool zinatarajia kupigwa faini Mei 19 mwaka huu na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), baada ya mashabiki wa timu hizo  kuonesha utovu wa nidhamu wakati timu zao zilipokutana kwenye mchezo wa marudiano hatua ya 16 bora, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Hatua hiyo ilitokana na mashabiki wa timu hizo kupigana baada ya mchezo kumalizika ambao uliifanya Liverpool kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1.
Tukio hilo lilitokea baada ya mashabiki wa Manchester United waliokaa upande wa mashariki kuanza kushangilia kwa kuichoma kwa moto bendera ya Liverpool.
Tukio hilo lilisababisha mashabiki wa Manchester United na Liverpool kuingia kwenye ugomvi ambao ulikuja kuingiliwa na polisi na kuwakamata mashabiki watano.
UEFA inatarajia kutoa adhabu hiyo Mei 19, mwaka huu, ambapo mashabiki wawili ni wa Liverpool na watatu kutoka Manchester United.