27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

LIPUMBA ASISITIZA KUMTAMBUA MAALIM SEIF

Na Asha Bani, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa,  Profesa  Ibrahim  Lipumba  amesisitiza kuwa bado anamtambua Maalim Seif Shariff Hamad kuwa ni Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Hata hivyo, amesema  Maalim Seif ni mtoro kazini.

Profesa Lipumba amemtaka katibu mkuu huyo kufika ofisi kuu za chama hicho  Buguruni,  Dar es Salaam kwa ajili ya kuendelea na kazi ambazo kwa sasa zinafanywa Naibu Katibu Mkuu  Bara, Magdalena Sakaya.

Alikuwa akizungumza jana katika mahojiano na Televisheni ya Star Tv.

Profesa Lipumba alisema licha ya hatua anazoendelea kuchukua katika chama hicho ikiwamo kuwafukuza wabunge wanane wa viti maalum, bado anamtaka Maalim Seif kufika ofisini Buguruni kwa ajili ya kufanya kazi.

“Sijamuona Maalim Seif tangu Agosti 23, 2015,  hivyo namtaka afike katika ofisi za Buguruni   aweze kupokea maelekezo ya kazi kutoka kwangu na aanze kazi,’’alisema Profesa Lipumba.

Julai 25, mwaka huu, Profesa Lipumba alimuandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu uamuzi wa aliloliita Baraza Kuu la CUF lililokaa na kukubaliana kuwafukuza wabunge wanane na madiwani wawili.

Wabunge hao ni   Severine Mwijage, Saumu Heri Sakala, Salma Mohamed Mwasa, Riziki Shaha Ngwali, Raisa Abdallah Mussa, Miza Bakari Haji, Hadija Salum Ally Al-Qassmy na Halima Ali Mohamed.

Katika barua yake   kwa Spika, Profesa Lipumba alisema alilazimka kuchukua hatua hiyo kwa sababu wabunge hao walikihujumu chama katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika Januari 22 mwaka huu, walimkashifu Lipumba na Sakaya na walishiriki katika kampeni ya Ondoa Msaliti Buguruni aliyosema ilipangwa na Chadema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles