25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MAKAMBA: TUTAIMARISHA FUKWE ZOTE ZA DAR

NA ASHA BANI

-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amesema fukwe zote za Mkoa wa Dar es Salaam zitaimarishwa   kuweza kuwa kivutio cha utalii na kuongeza pato la taifa.

Amewataka wanaojenga pembezoni mwa fukwe na vyanzo vya maji bila kufuata sheria ya mazingira kuondoka haraka iwezekanavyo kabla ya hatua hazijachukuliwa.

Makamba alitoa kauli hiyo   Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa uzio pembezoni mwa mito na bahari.

Alisema ujenzi huo umefikia asilimia 75 na mkataba wake ni wa miezi saba.

 

“Hatua ya ujenzi huu ni uimarishaji wa fukwe katika jiji hili na utakamilika Novemba kuchochea vivutio vya utalii na kuongeza pato la taifa,”alisema.

Akiwa katika mfereji mkubwa unaonganisha eneo la Buguruni  Malapa na Bungoni, alisisitiza mmiliki wa gereji kuondoka mara moja   kutoa nafasi   kwa ujenzi huo  unaoendelea.

“Sitaki kujua nani anamiliki hiyo gereji hapo nataka kuiona haipo kwa maana hapa tunatekeleza Sera ya Mazingira katika ofisi ya Makamu Wa Rais,” aliongeza Makamba.

Makamba pia alikagua ujenzi wa uzio wa bahari ya Hindi ambao umeanzia ufukwe  wa Coco Beach hadi pembezoni mwa Hospitali ya Ocean Road na kuelezea kuwa eneo hilo litakuwa la utalii zaidi.

Alisema eneo hilo litakuwa na kitega uchumi cha kutosha kwa kuwa litatumiwa kwa utalii na watu kupumzika.

Akiwa  katika  kingo  zilizopo pembezoni mwa  Chuo  cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, alisema  hata  wanafunzi na wakazi wa hapo wataishi kwa amani kutokana  na kingo za kuta kuacha  kuliwa na maji.

Msimamizi wa  mradi huo, Noela Shayo alisema   ukuta  wa Malapa utakua  na uimara kwa miaka  50 huku ufukwe wa Bahari ya Hindi utadumu  miaka 70.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles