22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Lipuli washusha kocha Mrundi

ZAINAB IDDY – DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Lipuli FC, umemtangaza Haerman Haruna , kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/20.

Katibu Mkuu wa Lipuli,Paul Leo, ameliambia MTANZANIA jana kuwa, kocha huyo raia wa Burundi atahudumu katika klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Alisema kuwa, pia mbali wamempa jukumu la kuwa kocha wa makipa, Riziki Shawa.

Alisema Shawa anauzoefu mkubwa kutokana na kuwahi kufanya kazi pia na klabu ya Simba.

“Tumeongeza makocha wawili, Haruna na Shawa ambao watasaidiana na aliyekuwa kocha wetu mkuu Samweli Moja ambaye msimu ujao atavaa viatu vya Selemani Matola kuwa msaidizi,”alisema.

Wakati huo huo, Leo alisema kikosi chao kiliondoka jana mjini Iringa kwenda Mbeya kwa ajili ya kucheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kurejea Iringa kwenye tamasha la klabu hiyo ambalo limepewa jina la ‘Lipuli Day’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles