26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Majeruhi wengine saba ajali ya moto waliolazwa Muhimbili wafariki

Christina Gauluhanga, Dar es Salaam

Majeruhi saba kati ya 32 wa ajali ya moto waliokuwa wanatibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo Agosti 15 na kufanya idadi waliofariki hadi sasa kufikia 21 huku wanaoendelea na matibabu wakiwa 25, 17 kati yao wakiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na 16 katika wodi ya kawaida.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Agosti 15, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma MNH, Aminiel Aligaesha, amesema hadi jana watu sita walikuwa wamefariki na tayari miili yao imesafirishwa mkoani Morogoro ndugu zao wamejitokeza kuwachukua.

“Serikali imeahidi wanaozikwa Morogoro itagharamia mazishi lakini kwa wanaotaka kwenda Mikoa mingine kama Moshi, Tanga wanajigharamia wao ila serikali itatoa sanda na sanduku tu,” amesema.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Msamvu mkoani Morogoro Jumamosi Agosti 11, na kusababisha vifo vya watu 89 na majeruhi zaidi ya 70.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles