LINAH HABADILI DINI SABABU YA MAPENZI

0
1460

Na BRIGHITER MASAKI

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Linah Sanga ‘Linah’, amesema si sawa kubadili dini kwa sababu ya mapenzi.

Akizungumza na MTANZANIA, Linah amesema hayo baada ya baba mtoto wake kuwa wa dini tofauti na yeye, hivyo amedai kama atabadili dini ni kwa sababu ya Mungu na si mapenzi.

“Unajua kiimani hutakiwi kufanya vitu juu juu, hata ukibadilisha dini ni kwa sababu ya Mungu si kwa sababu ya mapenzi, kwa upande wangu sikutaka kufanya hivyo.

“Kwa upande wa mume hawapo tayari mtoto wao abadili dini na hata kwetu pia hawapo tayari wakiniona nabadili dini, lakini maisha yanaendelea kila mmoja na dini yake,” alisema Linah.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here