MFALME WA ROCK AFARIKI DUNIA

0
711

MARNES-LA-COQUETTE, UFARANSA

MKONGWE wa muziki wa Rock na filamu nchini Ufaransa, Johnny Hallyday, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74, baada ya kusumbuliwa na saratani ya mapafu.

Kifo hicho kimetokea mapema jana na mke wake, Laeticia Hallyday, alikuwa wa kwanza kutoa taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii.

Staa huyo alitangaza kuwa anasumbuliwa na saratani tangu Machi mwaka huu na alianza kupatiwa matibabu lakini hali yake ilionekana kubadilika siku hadi siku.

“Johnny Hallyday ametuacha, ninaweka wazi taarifa hii nikiwa siamini kichwani mwangu. Lakini huo ni ukweli kwamba mume wangu hayupo tena na mimi,” alisema Hallyday.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here