27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Lilian awashukuru Watanzania

lilian_kamazimaNA MWANDISHI WETU

MREMBO aliyeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia yaliyofanyika juzi Sanya nchini China, Lilian Kamazima, amewashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono toka alipoanza safari yake ya urembo hapa nyumbani hadi kuingia kwenye kumi bora ya warembo wa dunia wenye mchango kwa jamii.

Akitoa shukrani zake, Lilian alisema licha ya kuwa mpweke ila sapoti ya Watanzania hasa kwenye mitandao ya kijamii katika upigaji kura ulimfanya ajihisi yupo nyumbani na kuna watu wengi nyuma yake wanaomuunga mkono.

“Nimefurahi sana kuingia ‘Top 10’ ya warembo wa dunia wenye mchango kwa jamii, hii imewezekana kwa sababu Watanzania walikuwa nyuma yangu kunisapoti, najua kuna warembo wengi waliwahi kufika huku lakini hawakufanya vyema, ila hii ni dalili ya ushindi kwa nchi yangu,” alishukuru Lilian.

Lilian aliingia kwenye orodha ya warembo 10 wa dunia wenye mchango kwa jamii kwa sababu ni moja ya wapiga kampeni maarufu waliosaidia wanawake wengi wa Tanzania kuufahamu ugonjwa wa fistula na tiba yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles