Lil Wayne apoteza fahamu

Lil Wayne
Lil Wayne
Lil Wayne

MIAMI, MAREKANI

RAPA Lil Wayne, ameendelea kusumbuliwa na tatizo lake la kupoteza fahamu kutokana na ugonjwa wake wa kifafa.

Msanii huyo jana alianguka na kupoteza fahamu kwa muda kutokana na ugonjwa huo ambao umekuwa ukimsumbua tangu akiwa na umri mdogo.

Mwaka huu amepoteza fahamu zaidi ya mara tatu na inadaiwa kwamba hali hiyo inatokana na matumizi mabaya ya pombe ambayo yanasababisha hali hiyo.

Hata hivyo, hali yake kwa sasa inadaiwa kuendelea vizuri lakini yupo chini ya uangalizi wa madaktari nyumbani kwake Miami nchini Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here