26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Baby J: Namtamani Yemi Alade

Jamilah Abdallah ‘Baby J’
Jamilah Abdallah ‘Baby J’

NA FESTO POLEA, ZANZIBAR

LICHA ya kushirikiana na wasanii mbalimbali wa muziki nchini, msanii wa muziki wa kizazi kipya visiwani Zanzibar, Jamilah Abdallah ‘Baby J’, ameweka wazi kwamba anatamani kufanyakazi na msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade.

Baby J aliyepata nafasi ya kutumbuiza katika ufunguzi wa Tamasha la Ziff kwa mwaka huu, alisema licha ya kushirikiana na wasanii wengi katika muziki wake lakini ndoto yake kubwa ni kuimba pamoja na mwanadada huyo wa Nigeria.

“Nampenda sana Yemi Alade, natamani siku moja tuimbe pamoja maana anajiamini, ana uwezo wa kucheza na jukwaa, kuimba na kufanya lolote kwa watazamaji kama nifanyavyo mimi naona tunafanana katika hilo ndiyo maana nampenda kufanya naye kazi,” alisema Baby J.

Baby J aliongeza kwa kuwataka wasanii kwa ujumla kujituma katika kazi zao na kutumia fursa ya tamasha la Ziff kwa ajili ya kukutana na wadau mbalimbali wa sanaa ya muziki katika kukuza muziki wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles