25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

LEMA KUSOMEWA MAELEZO YA AWALI KESI YA UCHOCHEZI

Na JANETH MUSHI, ARUSHA


MAHAKAMA ya Wilaya ya  Arusha, imepanga kumsomea hoja za awali Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), anayekabiliwa na shitaka moja la kuamsha hisia kwa wananchi kwa njia isiyo halali, baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Obadia Bwegoge, Wakili wa Jamhuri, Agness Hyera, aliiomba mahakama   kupanga tarehe ya kumsomea hoja za awali mshtakiwa huyo baada ya upelelezi wa shauri hilo namba 132 la mwaka huu  kukamilika.

Mbunge huyo anadaiwa kutenda kosa hilo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara Oktoba 22, mwaka 2016, katika eneo la Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro ambako inadaiwa alitoa maneno yaliyochochea hisia hasi kwa jamii kwa ngazi tofauti nchini.

Katika kesi hiyo, Lema anadaiwa kutamka kuwa Rais Magufuli akiendelea na tabia ya kudhalilisha demokrasia na uongozi wa upinzani, iko siku taifa litaingia kwenye umwagaji wa damu.

Pia, Lema anadaiwa kusema Rais yeyote ambaye haheshimu mipaka ya sheria, mipaka ya katiba, ataingiza Taifa katika majanga ya umwagaji damu, watu watajaa vifua, wakiamua kulipuka  polisi  wala jeshi halitaweza kudhibiti uhalifu utakaojitokeza.

Aprili 27, mwaka huu, Lema aliachiwa huru na mahakama hiyo chini ya kifungu cha 225 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai katika kesi ya uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli aliyokuwa akikabiliwa nayo baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuwasilisha  ushahidi.

Hata hivyo, baada ya kuachiwa huru, alikamatwa tena na kufunguliwa kesi hiyo moja ya kuamsha hisia kwa wananchi.

Katika kesi ya awali, namba 440 ya mwaka 2016, kabla mbunge huyo hajaachiwa huru, alidaiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Oktoba 22, mwaka 2016, katika eneo la Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro, kwamba alitoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles