Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini(LATRA) imewaagiza wasafirishaji wote wa abiria kwa mabasi kuzingatia masharti ya leseni za usafirishaji na matakwa ya Kanuni za Leseni za Usafirishaji.
Agizo hilo limetolewa leo Jumatatu, Januari 4, na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe kwa magari ya abiria
yaliyiotangazwa kwa tangazo na 76 kwenye gazeti la Serikali
Februari 7, 2020.
“Kanuni ya 4(2)(c); “Leseni ya kusafirisha abiria itatolewa kwa
muombaji aliyesajiliwa kwenye mfumo wa tiketi za kielektroniki ulioidhinishwa na Mamlaka.
“Kanuni ya 24(b)(d); “Msafirishaji mwenye leseni ya kusafirisha
abiria wa masafa marefu ahakikishe anatoa tiketi za
kielektroniki kwa abiria.
“Mamlaka inawataka wasafirishaji watoe tiketi za kielektroniki
kama kanuni zinavyoelekeza. Kuanzia Januari, 2021
hakuna msafirishaji atakayeruhusiwa kusafirisha abiria bila
kutoa tiketi za kielekroniki kwa abiria wote,” amesema Ngewe.
Amezitaja njia ambazo magari yake napaswa kutoa tiketi za kielektroniki kuwa ni:
“Dar-es-Salaam – Tanga, Tanga – Arusha, Dar es Salaam – Lindi,
Dar es Salaam – Mtwara, Dar es Salaam- Iringa, Dar es Salaam – Njombe, Dar es Salaam – Ruvuma, Dar es Salaam – Mbeya, Dar es Salaam-Tunduma, Dar es Salaam – Rukwa na Dar es Salaam – Morogoro.
“Nyingine ni Dar es Salaam – Kilombero, Dar es Salaam – Ifakara, Dar es Salaam – Malinyi na Dar es Salaam – Mahenge, maelekezo ya utekelezaji wa agizo hili kwenye njia nyingine yatatolewa hivi karibuni,” amesema Ngewe.