29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

LATRA Kilimanjaro yazipa kibali Coaster

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Kilimanjaro, imelazimika kutoa kibali kwa mabasi madogo ya abiria maarufu kama Coaster ya kukodi “Special Hire” ili kubeba abiria kuelekea Wilaya ya Rombo kutokana na wingi wa abiria kulikosababisha kuwa na uhaba mkubwa wa usafiri kwenye njia hiyo Jumapili iliyopita.

Mamlaka hiyo ilifanya ukaguzi kwa njia zote na kuelekeza mabasi kutoa kibali kwenye njia zenye uhitaji wa abiria wengi na kuchukua hatua kwa gari za ruti kuzidisha nauli na kuvunja sheria ya usafirishaji

Akizungumzia adha hiyo kwa waandishi wa habari Afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Nyello amesema katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi kuanzia Desemba 23-25 abiria ni wengi na magari hayatoshelezi mahitaji.

“Tarehe 23 na 24 abiria walizidi kushinda uwezo wa mabasi ya njia za Rombo na Tarakea ambapo ndipo kuna abiria wengi zaidi mamlaka imechukua hatua kwa kuchukua magari makubwa kama coaster za kukodi maarufu Special Hire na kupatana bei nafuu kwa abiria,” amesema Nyello.

“Amesema magari ya kukodi special hire yalitaka kuwabeba abiria katika njia hiyo kwa bei ya kupatana kwani yale magari yanasheria zake na utaratibu kutokana na yapo kwa ajili ya kukodiwa,” amesema.

Amesema mamlaka ikishirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani walikuwa stendi na kuhakikisha abiria wote wanapata usafiri.

Amesema kuwa mamlaka hiyo pia ilifanya ukaguzi kwenye magari yote ya ruti za ndani na kuhoji abiria kama wamezidishiwa nauli lakini hakukuwa na abiria yeyote aliyelalamika.

“Natoa wito kwa baadhi ya waandishi wa habari kuhakiki taarifa kutoka mamlaka kwa kupata ufafanuzi wa kina kwa kuwa wakati mwingine wanaotoa taarifa potofu kwa kutojua nini kinafanyika na mamlaka na sisi kuchukua taarifa upande mmoja,” amesema.

Upande wao, baadhi ya abiria wakizungumza kwa nyakati tofauti na wandishi wa habari wameshukuru LATRA kwa kusimamia vema suala la nauli kuwasaidia kuwapatia usafiri kutokana magari katika njia Rombo-Tarakea kutosheleza mahitaji yote ya abaria.

Abiria Amalia Shirima amesema kuwa usafiri wa Rombo ulikuwa shida lakini kulikuwepo watu LATRA ambao walituletea magari yale ya kukodiwa, kweli tunawashukuru walihakikisha tunasafiri salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles