Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
MBUNGE wa Viti maalumu, Agnesta Lambart alisimamisha Bunge kwa muda wa dakika tano baada ya kutoa hoja yake kuwa kubadili Taasisi ya Uhamiaji kuwa Jeshi kamili ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.
Aidha, mbunge huyo alisema ili kubadili taasisi hiyo kuwa jeshi kamili kuna kitu kinaitwa hati idhini ambacho kinatolewa na Amir Jeshi Mkuu ili waweze kubadili taasisi hiyo, lakini hakikufanyika.
Lambart alichangia mswada wa sheria ya uhamiaji jana bungeni jijini Dodoma alipokuwa akichangia mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 5 ya mwaka 2021.
Akitoa hoja yake mbunge huyo alisema kuwa kubadilishwa kwa Taasisi ya Uhamiaji kuwa jeshi kamili kunapingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ibara ya 28 kifungu cha 4 sura ya 54.
‘’Mheshimiwa Spika kitendo cha Uhamiaji kuibadili na kuwa jeshi kamili inakinzana na Katiba yetu ya nchi, katika kifungu kidogo cha 4, ibara ya 28 sura 54, kwani katiba ya nchi haiitambuia uhamiaji kuwa jeshi kamili bila kubadilisha jina,”amesema Lambart.
Aidha, mbuge huyo aliwataka wabunge hao kutafakari kwa kina kabla ya kuipitisha sheria hiyo kwani suala la jeshi ni suala la kikatiba hivyo waangalie kama wakipitisha isikinzane na Katiba ya inchi.
Alisema kufuta au kuanzisha jeshi kamili inatakiwa kuangalia Katiba pia, kwani Katiba ya muungano haitambui uhamiaji kuwa ni miogoni mwa majeshi ya nchi hii, ibara 147 kifungu kidogo cha (4).
Hata hivyo Mbuge huyo alisema endapo bunge hilo itaamua kupadisha uhamiaji kuwa jeshi kamili ili tuweze kuna mambo ya kufuatwa kabla ya uamuzi huo.
Baada ya kuona mbunge huyo kijana akiandamwa bungeni, Mbunge wa Viti maalum Halima Mdee (Chadema) alitoa taarifa kwa kunukuu taarifa ya kamati, Spika Ndugai alidakia na kuwambia “Halima kaa nchini, yale ni makosa ya kiuchapaji”.
Aidha, Lambart isema Rais wa Tanzania katiba inamtambua na kama kuna kitu hakiko sawa kuna kitu kinaitwa hati idhini tunahitaj hati idhini kutoka kwa amir jeshi mkuu.
“Sisi kamati ya sheria na katiba tulimuuliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili tupate hati idhini iweze kutuongoza lakini hatukupata majibu,” alisema .
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema suala la uhamiaji kuwa Jeshi kamili ni jambo la kawaiada kwani hata mataifa makubwa kama Uingereza, Marekani, India na Austrelia Idara ya uhamiaji ni jeshi kamili.
Wakati Mbunge huyo akiendelea kutoa mchango wake Spika Ndugai alikuwa akimkatisha mbunge huyo kwa kuuliza anachosema amekitoa katika kifungu gani cha katiba.
Licha ya Lambart kueleza na kutoa vifungu vya sheria lakini mchango wake ulikuwa ukikatishwa katishwa na baadhi ya wabunge walikuwa wakitoa taarifa.
Hata hivyo, kamati ya kudumu ya Katiba na Sheria ilitoa taarifa bungeni chini ya Mwenyekiti wake iliyosema melezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mbele ya kamati kuwa, hatua zote za kiserikali zilizingatiwa katika kufikia maamuzi ya Ibara ya 28(3) ya muswada huu.
Mwenyekiti huyo alisema; “Kuhusu kubadili hadhi ya Idara ya Uhamiaji kuwa Jeshi, busara za Kamati zimeona vyema Bunge lako Tukufu libaini maoni ya kamati kuhusu mazingira ya suala hilo kwa kuzingatia misingi ya katiba ya kwa ustawi wa taifa na kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo,”alisema.
Aidha mwenyekiti huyo alisema serikali ione umuhimu wa kutumia mfumo wa Hati Idhini ya Rais iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali, kama kiongozi Mkuu namba moja wa Sekta ya Utumishi wa Umma na Serikali kwa taasisi zote nchini, ambaye pia ndiye Kiongozi Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Alisema kuwa ili Hati hiyo iwe muongozo katika hatua zote za kubadili hadhi au muundo wa taasisi na vyombo vyote vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.